Skip to main content

KINANA KUSHAMBULIA MAJIMBO YOTE YA MKOA WA IRINGA

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliyevaa vazi la Kiislamu alipokuwa akitoa taarifa ya ujuio wa Kinana mkoani Iringa
Hassan Mtenga, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulaman Kinana atawasili mkoani Iringa Oktoba 6 katika ziara yake ya siku sita itakayompitisha katika majimbo yote ya mkoa wa Iringa.
Atakapowasili atalakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa wa Iringa wakiwemo wabunge.
Akizungumza na wanahabari hii leo, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema ziara ya Kinana itaanzia katika jimbo la Isimani kabla ya kwenda jimbo la Kalenga siku inayofuata.
Alisema baada ya kutoka Kalenga, atakwenda jimbo la Kilolo kisha kuelekea wilayani Mufindi atakakotembelea majimbo yote mawili, Mufindi Kusini na Mufindi Kaskazini.
Ziara ya Kinana itahitimishwa Oktoba 11, katika jimbo la Iringa Mjini linaloongozwa na Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.
Mtenga alisema ziara ya Kinana inalenga kuimarisha chama hicho, kusikiliza kero za wananchi na kutoa maelekezo muhimu yatakayosaidia kukijenga chama hicho.
Rai ya Chadema
Katika mkutano wake uliofanyika katika uwanja wa Kata ya Kihesa juzi, Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa alilitaka jeshi la Polisi kupiga marufuku aina yoyote ya maandamano itakayofanywa na wafuasi wa CCM wakati wa ziara yake hiyo.
Msigwa na viongozi mbalimbali wa chama chake walitoa rai hiyo baada ya jeshi la Polisi kuzuia msafara wa pikipiki, magari na maandamano yao yaliyokuwa yameandaliwa na wafuasi wa chama hicho wakati wakimpokea Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrick Ole Sosopi.
“Tumetii maelekezo ya Polisi, vijana wetu wa bodaboda wamezuiwa kutupokea; ili haki itendekea tunataka Kinana na timu yake watakapoingia mjini Iringa, misafara yao isiwe na maandamano ya watu, pikipiki wala magari,” alisema Mchungaji Msigwa katika mkutano wao mkubwa uliofanyika katika kata ya Kihesa mjini Iringa.
Taarifa ya CCM
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa alisema katika ziara hiyo chama hicho hakina mpango wa kufanya maandamano kwa kuwa huo sio utaratibu wake.
“Sisi sio watu wa maandamano, nanyi mnajua hivyo; Chadema ndio chama kinachoepnda kuandamana kwa kila jambo hata lisilo na maana kwa watanzania. Kinana anakuja Iringa ikiwa ni muendelezo wa ziara anazoendelea kufanya katika mikoa yote nchini, anakuja kujenga chama, atawakuta watu katika maeneo yao kwahiyo hatuna mpango wa kuwakusanya kwa maandamano,” alisema.
Aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika ziara hiyo inayotarajiwa kukiongezea nguvu zaidi chama hicho. CHANZO: BONGOLEAKS

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...