Skip to main content

MANISPAA YA IRINGA YAFUTA VIJIJI SABA



 Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo (kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuhuisha rejesta ya wakazi katika mitaa leo ofisini kwake. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Na Friday Simbaya, Iringa

Manispaa ya Iringa kupitia waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa imeridhia kufutwa kwa vijiji na kubakiwa na mitaa, hivyo Manispaa itakuwa na mitaa 192 kwa ongezeko la mitaa 43 (mitaa ya zamani 149).

Akiongea na waandishi wa habari leo  ofisini kwake Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema kuwa mitaa 14 iliyotokana na maombi ya kugawana mitaa iliyoonekana kuwa na eneo kubwa na mitaa 29 iliyotokana na vitongoji kuitwa mitaa kutokana na vijiji kufutwa.

Aidha, alivitaja vijiji saba (7) vilivyofutwa kuwa ni Igumbulo, Nduli, Kigonzile, Mgongo na Itamba. Katika tangazo la serikali namba 300 la tarehe 22.08.2012 limeelezea maeneo ya utawala katika mamlaka za serikali za mitaa mwaka 2014. 

Kwa kuzingatia tangazo hilo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imekubaliwa kuwa na kata 18, kata mpya zikiwa ni kata ya Igumbulo inayotokana na kugawanywa Kata ya Ruaha na Kata ya Mkimbizi ambayo imetokana na kugawanywa Kata ya Mtwivila.

Kuhusu kuhuisha rejesta ya wakazi katika mitaa mkurugenzi huyo aliwataka wananchi wote wa Manispaa ya Iringa wajitokeze kujiandikisha katika rejesta ya wakazi katika mitaa husika.

Alisema kuwa daftari la wakazi la mtaa ni kumbukumbu ambayo inataarifa zote muhimu za wakazi wa mtaa na vitongoji wa eneo husika. Taarifa hizo ni kama jina la mkazi, umri, mtaa anaoishi, idadi ya watoto kama wapo n.k.

“Rejesta ta wakazi ilianzishwa chini ya sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 ambapo inataka wakazi wote wawe wameandikishwa ikiwa umehamia, umehama au mtoto amezaliwa laizama taarifa ziwepo kwenye daftari la wakazi la mtaa,” alifafanua Mahongo.

Alisema umuhumu wa kuhuisha taarifa katika rejesta za wakazi pamoja na mambo mengine itasaidia kufahamu idadi ya wakazi katika kila mtaa, na itasaidia pia katika kuandaa mipango ya manispaa kwa kufahamu idadi ya wakazi ulionao na mahitaji yao katika mipango ya maendeleo.

“wanatakiwa kusimamia zoezi hili kwenye kata zetu ni watendaji wa mitaa na wa wenyeviti wa mitaa, kwani hawa ndio wanafahamu watu wake kwenye mtaa husika na ndio wanatambulika katika mfumo wa serikali kwenye ngazi ya mtaa,” alielezea.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...