Skip to main content

MKURUGENZI WA TFF MVELLA ATUPWA JELA MIAKA SITA











Mvella mwenye suti ya michezo siku moja kabla hajahukumiwa
MAHAKAMA ya Mkoa ya Iringa jana imemtia hatiani  Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Eliud Mvella baada ya kupatikana na makosa manne ya kuendesha biashara ya bima bila kibali.
Mvella aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi Mkoa wa Iringa kabla ya kutimkia CCM katika miaka ya karibuni na kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) alihukumia miaka sita au kulipa faini ya Sh Milioni 3 baada ya kupatikana na hatia ya kutenda makosa hayo.
Mvella aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) alikwepa kutumikia kifungo cha miaka sita jela baada ya kufanikiwa kulipa faini ya Sh Milioni 3 iliyolipwa kupitia risiti namba 3425607.
Mvella ambaye mjini hapa anajulikana zaidi kwa jina la Mahanji alifikishwa katika mahakama hiyo akituhumiwa kwa kosa la kwanza la kuendesha biashara ya bima bila kibali, pili kufanya shughuli za bima bila usajiri, tatu kuuza stika za bima za magari na kava noti bila kibali na nne kutoa risiti za bima bila kibali.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Ruth Massam alisema Mahanji alitenda makosa hayo Mei 25, 2013 katika jengo la Higlands hall kwa kutumia kampuni ya bima hewa iliyojulikana kama Emock.
Alisema katika kosa la kwanza, mahakama hiyo imemtia hatiani Mvella na imempa adhabu ya kifungo cha miaka miwili gerezani au faini ya Sh Milioni moja.
Kwa mujibu wa hakimu huyo, Mvella amehukumiwa miaka miwili gerezani au faini ya Shmilioni moja kwa kosa la pili na kifungo cha miaka miwili au faini ya Sh Milioni moja kwa kosa la tatu na nne.
Kwa kupitia kampuni hewa ya bima ya Emock, Mvella alitenda makosa hayo kwa kutumia kampuni ya Bima ya Mwananchi yenye makao yake makuu Arusha wakati hakuwa mwajiliwa wa kampuni hiyo.
Alisema mshakiwa alikutwa na vifaa vya kampuni hiyo kwenye ofisi iliyopo jengo hilo la Highland.
Hata hivyo ofisi hiyo haikuwa na kibao cha jina la  kampuni lakini risiti zake zilikuwa zikionesha kuwa inafanya kazi za Kampuni ya Bima ya Mwananchi.
Alisema Mvella alikuwa amewaajiri wanawake wawili kwa ajili ya utoaji wa huduma hizo za bima kwa kupitia kampuni hiyo hewa ya Emock.
Wakili wa Serikali Alex Mwita aliiomba Mahakama hiyo iangalie namna ya kumpunguzia adhabu mshitakiwa huyo kwa kuwa hajawahi kutenda kosa lolote.
Hakimu alitoa fursa kwa wakili wa utetezi, Erick Nyato ambaye alimwachia mshitakiwa ajitetee mwenyewe.
Mvella alisema anaomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa na ndugu wanaomtegemea akiwemo mama yake mzazi ambaye ana umri mkubwa na watoto wanaosoma shule na vyuo.
Alisema pia anafanya kazi za kijamii kupitia shirika la IYODEA (Iringa Youth Development Association). (BONGOLEAKS)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...