Skip to main content

MOI yajiimarisha katika utoaji huduma muhimu za Tiba na Upasuaji


Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Almas Jumaa akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi Taasisi hiyo ilivyoendelea kuwa nguzo Muhimu katika kuokoa maisha ya watanzania ambapo upasuaji wa kitaalam wa mgongo umeendelea kufanyika na kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 99 na kusaidia kuwaondoa wagonjwa wenye tatizo hilo katika hatari ya kupotea uhai.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi PICHA NA MAELEZO




Na Hassan Silayo-MAELEZO

Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeendelea kuwa nguzo muhimu nchini katika utoaji wa huduma za tiba na upasuaji.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Patrick amesema kuwa MOI imesaidia kuokoa zaidi ya asilimia 95 ya watanzania ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kupoteza maisha yao au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali.

“MOI kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuokoa maisha ya watanzania kwa zaidi ya asilimia 95 kutokana na kutoa huduma muhimu ya za tiba na upasuaji wa wagonjwa wanaopokelewa na hivyo kupunguza vifo na rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi” alisema Mvungi.

Akizungumzia kuhusu upasuaji wa kitaalam wa mgongo (specialized Spine Surgeries) Mvungi alisema kuwa Taasisi hiyo imeendelea kufanya na zaidi ya asilimia 99 ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wamepona na kurudi katika hali zao za kawaida.

Naye Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi Taasisi hiyo Bw. Almas Jumaa alisema kuwa zaidi ya wagonjwa 1,256 ya wagonjwa wa upasuaji mkubwa wa nyonga walipasuliwa salama na zaidi ya asilimia 95 ya wagonjwa hao wamepona kabisa.

Pia Almas alisema kuwa pia Taasisi imeendelea kutoa matibabu ya magonjwa ya ubongo yaliyokuwa yanahitaji upasuaji yamefanikiwa kufanyika kwa zaidi ya asilimia 80 na wagonjwa waliokuwa na matatizo hayo wamepona na kuondolewa kwenye hatari ya kupoteza uhai.

Taasisi ya MOI imewataka watanzania kuitumia Taasisi hiyo na kuacha kufuata matibabu nje ya nchi kwa gharama kubwa tofauti na kama wangepata huduma hizo hapa nchini kwa gharama nafuu.



Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...