Skip to main content

MSIGWA: KINANA AMETUSAIDIA KUPONDA MAWE MAGUMU

 Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dkt.Yahaya Msigwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Iringa kuhusu ziara ya siku sita ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyeifanya mkoani hivi karibuni. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dkt. Yahaya Msigwa amesema kuwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyeifanya mkoani hapa imesaidia kuponda mawe magumu na kutuachia mawe madogo madogo.


Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu mawe magumu hayo ndani ya chama katibu mwenezi huyo wa mkoa alisema kuwa ziara ya siku sita ya kinana kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zinakikabili chama hicho.

Alisema kuwa kiongozi huyo wa kitaifa aliwapa fursa wananchi kuuliza maswali ambayo yamesadia kuibua changamoto mbalimbali na wao kama chama mkoa kero hizo wanaendelea kuzifanyia kazi.

“Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye walikuwa katika ziara ya siku sita mkoani Iringa kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi,” aliongeza katibu mwenezi wa mkoa huyo.

Aidha, katibu mwenezi huyo wa mkoa alisisitiza viongozi kuwa karibu na wananchi ili kuweza kusikiliza matatizo yao kuliko kukaa ofisini kuhusu kuletewa kero hizo ofisini.

Alisema kuwa katibu mkuu kinana alisisitiza umuhimu wa kuweka viongozi wanaokubalika na wananchi pamoja kuheshimu moani ya wananchi ili kusimamisha viongozi  wanaokubalika  kwa kufuata katiba, kanuni na taratibu za chama.

Wakati huohuo, Katibu Mwenezi CCM Mkoa, Dkt. Msigwa aliwaasa wananchi kujiandikisha katika daftari ya mpigakura ili wawezekushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ule Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Alisema kuwa ni lazima wananchi wa hakikishe wanachagua viongozi wazuri wanaotokana na chama cha CCM ili kuweza kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu  kama tunu aliyetuachia Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.
 




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...