Skip to main content

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AUAWA KISHA KUPORWA PIKIPIKI



Kamanda wa Polisi mkoani Iringa (RPC),Ramadhani Mungi

Na Friday Simbaya, Iringa
 Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lugalo ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiofahamika kisha kupora pikipiki yake ambayo haijafahamika namba za usajili.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa (RPC),Ramadhani Mungi amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake leo kuwa Salehe Khamis (18) aliuawa tarehe 06/10/2014 majira ya saa 6:15 usiku katika Kitongoji cha Kikungwe Igumbilo, Kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa.
RPC alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni pamoja na kuwania mali, ambapo hata hivyo, watuhumiwa wanatafutwa na jeshi la polisi.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia dereva mmoja wa lori aina ya Isuzu kwa kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu huko katika Kijiji cha Itimbo Kata ya Ihimbo, Tarafa ya Kilolo mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alimtaja marehemu kuwa ni Linus Mwirafi (45) mkazi Kijiji cha Itimbo aliyedondokewa na lori hiyo baada ya kupinduka.
Alisema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 244 CNK aina ya Isuzu likiendeshwa na Yoktani Kikula (25) mkazi wa Ipogolo lilipunduka na kumdondokea mtembea kwa miguu huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.
RPC alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 05/10/2014 majira 06:00hrs katika kijiji cha Itimbo wilayani Kilolo, mkoani Iringa, na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva amekamatwa.





Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...