Skip to main content

NAPE: JIMBO LA IRINGA MJINI MPANGAJI WAKE KODI YAKE IMEKWISHA

Kamanda wa UVCCM mkoa  wa Iringa Bw  Salim Asas  akisalimiana na katibu wa itikadi na uenezi Taifa  Nape Nnauye  leo 
Vijana  wa CCM  wakijiandaa kumvisha skafu katibu mkuu wa CCM taifa Bw Kinana  leo baada ya  kuwasili  Iringa kwa ziara ya  siku 6 
Kinana  akivishwa  skafu  
Mbunge wa  jimbo la Isimani  Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya  waziri mkuu  sera na uratibu wa bunge  kulia akisalimiana na katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana lea  baada ya  kuanza  ziara yake  wilaya ya Iringa 
Mbunge wa  jimbo la Kilolo na Prof Peter Msolla  kulia akisalimiana na Kinana 
Kinana  akisalimiana na viongozi wa CCM wilaya ya Iringa 
Kamanda wa UVCCM mkoa  wa Iringa Bw  Salim Asas  akisalimiana na katibu wa itikadi na uenezi Taifa  Nape Nnauye  jana.
Mdau wa matukiodaima Bi Shirima  akisalimiana na Kinana  leo 
kada wa CCM jimbo la Iringa mjini Dr Yahaya  akisalimiana na Kinana 
wana CCm wakiwa katika  viwanja vya CCM wilaya ya Iringa  vijijini leo 
Nape  kulia akiwa na  wana CCM Iringa  leo 
Wana CCM wakiwa katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa vijijini leo 

Askari  wakiwa katika  ulinzi mkali 
Kinana  akifungua ofisi ya  CCM wilaya ya Iringa  vijijini baada ya  kukarabatiwa  upya 

 

KATIBU  wa  itikadi na uenezi  wa chama  cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape  Nnauye  ambana mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amfananisha na mpangaji na  kuwa kodi yake ya  kuendelea kudumu katika  jimbo  hilo  imekwisha  hivyo ajiandae  kufungasha vilago ili  uchaguzi mkuu 2015 akabidhi jimbo hilo CCM.

Nnauye  alitoa kauli hiyo  JANA  mara  baada ya  kuwasili katika  jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya  ziara siku 6 mkoani Iringa na  katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana.

" Tutakuwa na  ziara  mkoa wa Iringa kwa muda wa  siku  6 na hadi  tukimaliza  ziara  yetu hapa  Iringa  chama  chetu  kitakua  juu  zaidi hivyo  nawaombeni fikisheni  salamu kwa  wapangaji kuwa kodi yao  imekwisha  na  hivyo  tunahitaji watuachie jimbo  letu na  kwa sasa  hatuna mpango wa kupangisha   tena," alisema Nnauye  huku akishangiliwa na umati wa  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  waliokuwepo katika mapokezi hayo.

Akizungumza na  wanachama   hao  kabla ya  kuzindua  ofisi  ya CCM wilaya ya  Iringa  vijijini  Iliyofanyiwa  ukarabati upya katibu  mkuu, Abdulrahman Kinana alisema  kuwa CCM imeendelea  kukamilisha utekelezaji wa ahadi zake  ambazo ziliahidiwa  mwaka 2010  na  kuwa  hadi sasa  sehemu kubwa ya ahadi hizo  imetekelezwa na kilichobaki ni  kuwaomba  watanzania  kuendelea  kuwa na imani na CCM ili mwakani 2015  kuendelea kuchagua chama  hicho.

Kinana  alisema  kuwa  kazi  kubwa  imeendelea  kufanywa na  viongozi wa  CCM na  serikali yake  chini ya Rais Jakaya  Kikwete  katika  kuona  watanzania  wanaendelea kunufaika na matunda  ya serikali yao kwa kusogezewa  maendeleo karibu  zaidi na kutaja  miradi mkubwa ambayo imetekelezwa  kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara  za lami  kila kona ya nchi  hii.

" Tunazunguka  kuendelea  kukijenga  zaidi  chama lengo ni kuona  watanzania wanaendeleo kukiamini chama na  kuhamasisha  zaidi wananchi kujitokeza  kwa  wingi  katika chaguzi za  serikali za mitaa mwaka huu  ili  kuchagua  viongozi  wanaotokana na  CCM kwani ndicho chama  chenye mapenzi ya kweli ya  kuliongoza Taifa hivyo  hakuna  sababu ya  watanzania  kutokiamini  chama cha mapinduzi"

Pia alisema  kuwa mbali ya  CCM kuendelea  kukamilisha utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi bado chama  hicho kina mpango mzuri wa  watanzania  ili kuona mwakani 2015 chama  kinashinda na hapa  watanzania  wategemee  ahadi  nyingi  na kubwa zaidi  ya zile za mwaka 2010.

Awali  Kinana alimpongeza  aliyekuwa mjumbe wa  bunge malum la katibu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  kwa  jinsi  alivyowawakilisha  vema  wakazi wa mkoa wa Iringa na  watanzania kwa ujumla  na kuwa alikuwa akimfuatilia na kufurahishwa na uwezo wake mkubwa wa  kujenga  hoja.

Kwa upande wake Msambatavangu  akimkaribisha katibu mkuu  huyo alisema  kuwa  mbali ya  kuwa  ziara  hiyo inaanzia jimbo la Kalenga kwa upande wa wilaya ya Iringa vijijini ila mbunge  wake Bw Godfrey Mgimwa hatafanikiwa  kushiriki kutokana na heshima kubwa ambayo spika wa bunge Anne Makinda   amempa mbunge huyo kwa kumteua kuwa miongoni mwa  wabunge  wachache vijana kwenda  nje ya Tanzania  kushiriki mkutano mkuu wa dunia wa  wabunge  vijana. (MZEE WA MATUKIO DAIMA)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...