Skip to main content

NHC IMEZITAKA HALMASHAURI ZA MIJI ZITOE ARDHI KWA GHARAMA NAFUU




http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/08/Katanga-8.png


 http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/08/Katanga2.png
 Baadhi ya makazi duni eneo la Katanga nchini Uganda. (PICHA KWA MSAADA WA MTANDAO)


Na Friday Simbaya, Iringa
Ikiwa ni katika  kuaadhimisha siku ya makazi duniani Shirika la nyumba la taifa (NHC) katika juhudi ya kuunga mkono serikali ili kuondokana na makazi duni nchini lina mpango wa kujenga jumla ya nyumba 15,000 mpaka kufikia mwaka 2014/15.

Akiongea na THE SCOOP kwa njia ya simu Meneja wa Huduma kwa Jamii (CSR), Muungano Saguya alisema shirika la nyumba lina mpango wa kujenga jumla ya nyumba 15,000 ambapo nyumba 5,000  kati hizo zitakuwa za gharamu nafuu, wakati nyumba 10,000 zitakuwa za bei ya kati na juu.
Alisema mpaka sasa shirika limeshajenga jumla ya nyumba 1,227 za gharama nafuu na kuongeza kuwa Tanzania ina uhaba wa  makazi 3,000,000 kwa ongezeko  laki mbili kwa kila mwaka.
Alisema kuwa kuboresha makazi mijini shirika limejikita zaidi kwenye uboreshaji makazi mijini (urban renewal) kwa kubadilisha taswira za miji nakuifanya iwe namuonekano mpya.
“Hii ni pamoja na kubomoa majengo ya zamani na kujenga majengo mapya yenye viwango vyote vya usalama (safety),” aliongea meneja wa huduma kwa wateja huyo.
Kauli mbiu ya siku ya makazi duniani mwaka huu ni; Sauti kutoka makazi duni. 
Shirika katika kutatua tatizo la uhaba wa makazi nchini unakadiriwa kufikia nyumba 3,000,000 kwa kujenga nyumba bora, nafuuna za kisasa zitakazosaidia kupunguza upungufu wa makazi na kuleta mandhari bora mijini.
Hata hivyo, meneja wa huduma kwa jamii wa shirika la nyumba taifa alitoa rai kwa halmashauri za miji kutoa ardhi kwa gharama nafuu ili iweze kujenga nyumba bora na nyingi zaidi.
Siku ya makazi duniani uadhimishwa kila jumatatu ya kwanza ya mwezi oktoba kila mwaka. 
Na nchi wanachama wa umoja wa mataifa chini ya uratibu wa shirika la makazi duniani (UN-HABITAT) huadhimishasiku hii kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafakari hali ya makazi katika nchi husika na kupanga mikakati ya kukabiliana na changamoto za makazi.




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...