Skip to main content

NYALANDU: HAIWEZEKANI KILA MWANA MUFINDI KUVUNA MITI SAOHILL

Nyalandu katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Igowole, Mufindi Kusini, mkoani Iringa
Alisistiza mengi
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema haiwezekani kila mwananchi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa anayeomba kuvuna miti katika msitu wa Taifa wa Saohill ulioko wilayani humo akapata kibali.
“Nitakuwa muongo nikitoa ahadi hiyo; lakini niwaahidi tu kwamba tutazidi kuboresha kanuni zinazotumika kutoa vibali kwa waombaji ili rasilimali hii inufaishe watu wengi zaidi,” alisema.
Aliyasema hayo juzi katika ziara yake aliyoifanya katika kijiji cha Igowole wilayani humo akiitikia wito wa mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, Mendrad Kigola aliyemuomba waziri huyo kukutana na wananchi wa jimbo hilo ambao ni sehemu ya wadau wakubwa wa msitu huo.
Kwa kupitia risala yao iliyosomwa na Precious Nyalusi, wajasirimali wa jimbo hilo walimwambia waziri huyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa kijiji hicho kwamba walitegemea msitu huo ungewanufaisha zaidi watu wa Mufindi tofauti na ilivyo sasa.
“Tulitegemea tungekuwa wanufaika wa kwanza wa malighafi hii kwa kuwa umependwa katika meneo yaliyoachwa kwa nia njema na wazazi wetu, cha kushangaza unanufaisha zaidi matajiri, wakubwa na kampuni hewa” alisema.
Awali Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini alimueleza waziri huyo kwamba msitu huo ni sawa na mali ya wana Mufindi kwa kuwa wao ndio waliopanda na kuulinda hadi kufikia hatua ya kuvuna hivyo kuna kila sababu  asilimia 50 ya kila mgao unaotengwa kwa ajili ya uvunaji kila mwaka ikatolewa kwao.
“Mwaka jana asilimia 52 ya mago ulitolewa kwa wazawa huku asilimia 48 zikitolewa kwa wageni; Mwaka huu Mufindi Kusini tulichopata hakizidi asilimia tano,” alisema.
Kigola alisema; “sina matatizo na jinsi Mamlaka ya Misitu Tanzania ilivyotoa mgao kwa vijiji na baadhi ya wananchi, shida yangu iko kwenye mgao wa vikundi hasa vya wilaya ya Mufindi,” alisema.
Alisema wakati vikundi 12 vya jimbo la Mufindi Kusini ndivyo vilivyopata mgao, 36 vilivyobaki vimetoka katika jimbo la Mufindi Kaskazini linaloongozwa na Naibu Waziri na Utalii, Mahamudu Mgimwa.
Katika majibu yake Nyalandu aliwapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwanza kwa kutoa maeneo yao yaliyopandwa masitu huo na pili kwa kuulinda msitu wenyewe.
Alisema ili kuwafanya watanzania wengi wanufaike na rasilimali hiyo, serikali iliamua kusitisha maamuzi yake ya kuuza miti katika misitu yake kwa njia ya mnada na kuendelea na mfumo wa sasa wa vibali.
“Zilikuwa ni busara za Rais jaka Kikwete, vinginevyo rasilimali hii ingekuwa inawanufaisha wenye uwezo mkubwa wa kifedha kwasababu katika mnada anayetoa zaidi ndiye anayeuziwa,” alisema.
Alisema kwa kupitia mfumo wa vibali, yapo baadhi ya maeneo yanahitajika kuboreshwa  ili kuwafanya watanzania wengi zaidi na wale wanaosaidia kulinda misitu wanufaike.
“Kama nilivyosema haitawezekana kila mwana Mufindi au wadau wote wanaoomba mgao wa kuvuna watapata kibali lakini tutakachofanya ni kuyakumbuka maeneo yote ambayo wananchi wanatusaidia kulinda misitu,” alisema.
Aliiagiza Mamlaka ya Misitu Tanzania (TFS) kuendelea kuboresha kanuni zinazotumika kutoa vibali kwa waombaji wakizangatia maslai mapana ya Taifa.
“TFS waangalie sehemu zote zinazotatanisha  katika mfumo wa mgao tunaotumia sasa, yaliyojitokeza yasipuuzwe, pitieni upya taratibu za utoaji wa vibali ili makundi yote yanufaike; wananchi, viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, vikundi vijiji, taasisi na wadau wote  kwa kadri itakavyowezekana wakumbukwe lakini kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria,” alisema. CHANZO: BONGOLEAKS

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...