Skip to main content

OFISI YA WAZIRI MKUU YAFANYA TATHIMINI YA HALI YA CHAKULA NA LISHE MKOANI SIMIYU

Bw. Clement Ngosha wa kijijini Kabita Wilayani Busega, Simiyu, akitumia mbegu za mahindi kueleza hali ya chakula kijijini hapo kwa wataalam wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Oktoba, 2014.

Mtaalam wa Usalama wa chakula kutoka Wizara ya kilimo, chakula na Ushirika, Bi. Tatu Kayumbu akiihoji moja ya kaya kijijini Mwamanyili,Wilayani Busega, Simiyu wakati wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kijijini hapo, Oktoba, 2014.





Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Kabita wilayani Busega, Simiyu wakifuatilia mkutano wa kijiji uliokuwa ukijadili hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipofika kijijini hapo kufanya tathmini ya masuala hayo Oktoba, 2014.



Na Ibrahim Hamidu

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa maafa inafanya Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe Mkoani Simiyu katika Wilaya zake zote ambazo ni; Halmashauri za Wilaya za Bariadi, Itilima, Maswa ,Bariadi Meatu na Busega.

Akiongea mkoani Simiyu kiongozi wa Wataalam wa tathmini ambaye pia ni mratibu wa shughuli za maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Edgar Senga alibainisha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imefikia maamuzi hayo ya kufanya tathmini mkoani Simiyu baada ya mkoa huo kutuma maombi katika Ofisi hiyo kuwa wana upungufu wa chakula.

“ Ofisi ya mkoa ya Simiyu ilileta maombi kwa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa wanaoupungufu wa chakula takribani tani 48,975, kwa kuwa Ofisi yetu ndio yenye dhamana ya kuratibu misaada ya chakula hivyo haikuwanabudi kufanya tathmini ya haraka ili kubaini hali ya chakula ya mkoa huu ili kuweza kuamua namna ya kushughulikia maombi yao ya msaada wa chakula” alisema Senga.

Senga alibainisha kuwa Wataalam wa tathimini hiyo wanatoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika katika Idara ya Usalama wa Chakula ambao kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu wametawanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu ambapo katika kila Wilaya vitachaguliwa vijiji vitatu vya kufanyiwa tathmini.

“Katika kila kijiji wataalamu hawa watakuwa wanamadodoso ya Wilaya na kijiji ambayo yatasaidia kutoa taarifa mahsusi za hali ya chakula na Lishe katika ngazi ya Wilaya na Kijiji, lakini pia wataalamu wanayo madodoso ya kaya ambayo yanalenga kupata taarifa za hali ya chakula na Lishe kwa kaya husika kwa vijiji vitakavyoteuliwa na Serikali za vijiji hivyo. 

Kwa kuzingatia kuwa wataalam wa masual ya chakula katika ngazi ya Wilaya watakuwa wanahusishwa ninaamini tutapata taarifa bora ya hali ya chakula ya mkoa wa Simiyu ” alisisitiza Senga.

Akiongea Ofisini kwake alipotembelewa na ujumbe wa Wataalamu hao Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) mkoani Simiyu, Bw. Joseph Nandira alibainisha kuwa Katika kipindi cha msimu wa 2013/2014, Mkoa ulijiwekea malengo ya kuzalisha jumla ya tani 1,003,578 za mazao ya chakula aina ya nafaka/wanga na tani 150,257 aina ya mikunde. Mavuno halisi yaliyopatikana ni tani 476,024 za chakula aina ya nafaka/wanga na tani 74,944 za chakula aina ya mikunde.

Nandira alibainisha kuwa kutokana na tabia ya wananchi kuuza sehemu kubwa ya chakula ili kukidhi mahitaji ya familia zao, tathmini ya hali ya chakula tuliyoifanya mwezi Julai 2014, tulibaini kuwa Mkoa Unaupungufu wa chakula wa tani 48,975 za nafaka ambao umeanza kuanzia mwezi Oktoba na upungufu huo wa chakula unatarjiwa kuwepo mwezi Novemba/Desemba hadi Februari, 2015 kama wilaya hazitapata msaada wa chakula.

“Tathmini hiyo ilibaini Halmashauri za Wilaya za Busega na Meatu zina upungufu wa chakula kuanzia mwezi Agosti, 2014 hadi Februari, 2015. Halmashauri za Wilaya za Bariadi, Itilima, Maswa na Bariadi Mji zina upungufu wa chakula kuanzia mwezi Oktoba, 2014 hadi mwezi Februari, 2015. Ili kukidhi haja ya upungufu wa chakula ndio maana tuliomba jumla ya tani 48,975 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.” Alisema Nandira.

Nandira alifafanua kuwa ili kuhakikisha tatizo la upungufu wa chakula linakwisha tayari mkoa unayomikakati ambayo inajikita katika Kuwahimiza wananchi kutumia vizuri chakula kilichopatikana na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima. 

Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu makadirio ya mahitaji ya chakula ngazi ya kaya kwa mwakapamoja na Kuwashauri wananchi kuuza sehemu ya mifugo yao na kujinunulia chakula wakati huu ambapo chakula bado kina bei ndogo na kinapatikana ndani ya Wilaya na Mkoa.

Aliongeza kuwa mkoa unaendelea kuwashauri wananchi kujinunulia chakula kutokana na fedha za mauzo ya pamba. Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu hifadhi bora ya chakula, ikiwa ni pamoja na matumizi ya vihenge bora/vya kisasa na madawa ili chakula kisibunguliwe na wadudu. Kuwashauri wananchi kuuza ziada ya chakula walichovuna na si vinginevyo.

Kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2012 mkoa wa Simiyu una jumla ya watu 1,584,157 ambao wanahitaji jumla ya tani 404,752 za chakula aina ya nafaka/wanga na tani 144,553 za chakula aina ya mikunde kwa kipindi cha msimu wa mwaka 2013/2014. 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...