Skip to main content

PHIRI ATAMBA KUSHINDA JUMAMOSI

Rais wa timu ya Lipuli Jesca Msavatavangu (mwenye kapelo) akisalimia na kikosi cha Lipuli kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Simba SC ya Dar es Salaam jana katika uwanja wa samora mjini Iringa, ambapo Simba ilishinda goli 1 kwa nunge. (Picha na Friday Simbaya)

Na Friday Simbaya, Iringa


Timu  ya Simba ambayo inajiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Suger ya Mkoani Morogoro,  siku ya Jumamosi  imeonja ladha ya ushindi  baada ya kuifunga timu ya Lipuli (Wanapaluhengo)  ya mkoani Iringa ambayo ipo kwenye maandalizi ya mechi ya ligi daraja la kwanza dhidi ya Kimondo Fc ya Mkoani Mbeya.


Mchezo huo ulimalizika kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa nunge, mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Kumbukumbu Samora mjini Iringa.

Timu ya Simba  ambayo imeshuka dimbani  mara  tano kwenye ligi kuu Tanzania Bara msimu huu na kutoka sare michezo yote huku ikiwa imefunga goli tano na kufungwa  idadi hiyo, inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kocha wa timu ya SIMBA Mzambia  Patrick Phiri, aliutumia mchezo wa jana kama maandalizi,huku akiwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha vijana cha  timu hiyo.

Timu ya SIMBA ilianza mchezo taratibu na kuifanya timu ya Lipuli kutawala kipindi cha kwanza ambapo hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana.

Kipindi cha pili Simba walionekana kubadilila na kuanza kulishambulia kwa kasi lango la lipuli hatimaye ilifanikiwa kupata goli ambalo lilifungwa na mshambuliaji hatari Elias Maguli ambae alitumia makosa ya mabeki wa Lipuli waliochelea kuondoa mpira kwenye eneo lao la hatari.

Kuingia kwa bao hilo kuliufanya mchezo kuchangamka huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini mpaka mwisho wa mchezo Simba waliibuka kifua mbele.

Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo kocha mkuu wa Wekundu wa msimbazi akiongea na Waandishi wa habari alitamba kuibuka na ushindi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa akisema vijana wake wameahidi kushinda mchezo huo.

Kuhusu kupewa mechi mbili na uongozi wa timu hiyo kocha uyo alisema yeye kwa sasa anaangalia namna ya kushinda michezo yote iliyobaki.

Pia kocha huyo aliimwagia sifa timu ya Lipuli na kusema ni timu nzuri na wametoa upinzani mkali kwa vijana wake.

Kwa upande wake Rais wa timu ya Lipuli Jesca Msavatavangu alisema vijana wake walicheza vizuri huku wakionekana kucheza kwa hali na mali, hivyo kutoa burudani kwa wakazi wa Mjini Iringa na viunga vyake.

Msavatavangu alisema hiyo ilikuwa ni nafasi kwa vijana wake kuonekana kwa wakazi wa Iringa ikiwa ni pamoja na kuonyesha kiwango cha soka, kwa kucheza na timu kubwa zinazoshiriki ligi kuu.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...