Skip to main content

RAIS KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO

Waziri Pinda
*Azindua jengo la kisasa la Mama Ngojea wilayani Urambo

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka viongozi wa mkoa wa Tabora wajipange vizuri na kuhakikisha kuwa wanajenga vituo vya afya katika kila kata za wilaya ya Urambo kwa sababu bado iko nyuma.


“Hatua hii itasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali ya wilaya ya Urambo kwa sababu yenyewe imekuwa ndiyo kimbilio la kila mgonjwa kwa sasa,” amesema.

Ametoa agizo hilo  jana  wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Urambo mara baada ya kuzindua jengo la Mama Ngojea linaloitwa Mayu Lindila lililopo kwenye hospitali ya wilaya hiyo.

“Wilaya yenu ina kata 16, ina vijiji 57 na zahanati 22 lakini ina kituo kimoja tu cha afya. Na hii maana yake ni kwamba kuna vijiji havina zahanati kabisa. Huu ni mtihani mkubwa na ndiyo maana kila mtu akiumwa anakimbilia kwenye hospitali ya wilaya,” alisema Waziri Mkuu.

“Kisera kila kata ni lazima iwe na kituo cha afya, kwa hiyo viongozi wa mkoa na wilaya ni lazima mjipange kuona ni kwa namna gani mtaitekeleza sera hii, na pia jengeni zahanati kwenye vijiji ambavyo havina zahanati,” alisisitiza.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa huduma ya Mama Ngojea, Waziri Mkuu alisema unasaidia kuokoa maisha ya mama mjamzito anayetoka kata ya mbali ambaye anakabiliwa na tishio lakini siku zake za kujifungua zinakuwa hazijafika.

Alisema kutokuwepo kwa majengo ya Mama Ngojea katika maeneo mengi ni changamoto kubwa na hatari kwa akinamama wengi hasa waishio mbali na huduma za tiba. “Hivi kama kata moja iko mbali na makao makuu ya wilaya, na mama mjamzito mwenye tatizo hawezi kufika hospitali unadhani ataenda wapi? Si ataenda kwa wakunga wa jadi au waganga wa kienyeji tu?”

Aliwasihi akinamama wa wilaya hiyo wajitahidi kutumia huduma za hospitali kwa sababu kwa wakunga wa jadi na waganga wa kienyeji hakuna wataalamu kama waliopo hospitalini.

Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bibi Fatma Mwassa afanye utaratibu ili kila wilaya pawe na Mama Ngojea. “Hata kama hakuna hospitali ya wilaya lakini pana kituo cha afya, ni vema pawe na jengo la Mama Ngojea ili kuokoa maisha ya akinamama.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Kheri Kagya alisema jengo hilo lenye uwezo wa kulaza wagonjwa 24 kwa wakati mmoja, lilianza kujengwa Agosti 25, 2012 na lilikamilika Novemba 10, 2013 kwa gharama ya sh. milioni 198/-. Lina jiko, sehemu ya kulia, mabafu, vyoo, eneo la kufulia na kupumzikia.

Lengo la kujenga kituo hiki ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 228 kwa kila vizazi hai 100,000 na kufikia vifo 90 kwa kila vizazi hai 100,000 au chini ya hapo ifikapo mwaka 2015. “Mwaka 2012 tulikuwa na vifo 253 kwa kila vizazi hai 100,000 na mwaka jana tulikuwa na vifo 228 kwa kila vizazi hai 100,000. Nia yetu ni kupunguza kabisa vifo vya akinamama kabla na wakati wa kujifungua,” alisema.

Aliwashukuru Mbunge wa jimbo la Urambo ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta na mkewe Mama Margareth Sitta (ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa huo) kwa kubuni wazo hilo na kutafuta fedha za kujenga Mama Ngojea kwenye hospitali ya wilaya hiyo.

Wakati huohuo, Bwana na Bibi Sitta wamechangia mablanketi 300 na vyandarua 100 kwa ajili ya Mama Ngojea pamoja na hospitali ya wilaya hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...