Skip to main content

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa


 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) bw. Juma Reli akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari za Fedha na Uchumi (hawapo pichani)  wakati wa ufunguzi wa semina hiyo leo mjini Bagamoyo,Mkoani Pwani,Kulia ni Mwenyekiti wa washiriki hao Bw. Thomas Chilala na Kushoto ni Meneja Uhusiano na Itifaki wa Benki Hiyo Bi Zalia Mbeo.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) bw. Juma Reli wa tano kutoka kulia (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari za fedha na uchumi mara baada kufungua semina iliyoandaliwa na Benki hiyo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kuelimisha wananchi ili waweze kutumia fursa zilizopo ikiwemo kushiriki kununua dhamana za Serikali.

Frank Mvungi- Maelezo, Bagamoyo

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa za Uchumi na fedha kwa wananchi ili kuongeza wigo wa wananchi kushiriki katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo endelevu.

Hayo yamesemwa leo mjini Bagamoyo na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Juma Reli wakati akifungua Semina kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha iliyoandalliwa na Benki hiyo.

Akifafanua Bw. Reli amesema waandishi wa habari wanalo jukumu la msingi la kuuhabarisha umma kuhusu majukumu ya Benki hiyo katika kukuza uchumi na fursa zinazotolewa na Serikali ili kuwanufaisha wananchi.

“Navipongeza Vyombo vya habari hapa nchini kwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za uchumi na fedha kwa wananchi” alisema Reli.

Akizungumzia Lengo la Semina hiyo Reli amesema imelenga kuwaongezea ujuzi na weledi waandishi hao ili kuwasaidia wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo na namna wanavyoweza kunufaika nazo.

Naye Meneja Uhusiano na Itifaki wa BOT Bi. Zalia Mbeo alisema kuwa mwaka huu waandishi wa habari wapatao 20 wanashiriki katika Semina hiyo ambapo mwaka jana ilifanyika kwa mara ya kwanza na ilihusisha waandishi wa habari 15.

Pia bi Mbeo alisema BOT itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari hapa nchini kwa kuwa ni wadau muhimu katika kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu Kazi zinazotekelezwa na Benki hiyo kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.


Mada zitakazotolewa katika Semina hiyo ni pamoja na Ushiriki wa wananchi katika dhamana za Serikali,Soko la pamoja kwa nchi za Jumuiya Afrika Mashariki,Kurugenzi ya uchumi na Sera,Kurugenzi ya huduma za Kibenki na Sarafu,Kurugenzi ya usimamizi wa Mabenki,Kurugenzi ya Mifumo ya malipo na Bodi ya Bima ya Amana.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...