Skip to main content

Vijiji 1,800 kupata mawasiliano ya simu, internet mwakani

Dar es Salaam. Jumla ya vijiji 1,800 vinatarajia kupatiwa mawasiliano ya simu ya na teknolojia ya mawasiliano ya habari na mawasiliano (Tehama ) ifikapo mwakani.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Tehama wa Africa (Capacity Africa), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba alisema kuwa mpango huo upo katika hatua za mwisho na ifikapo mwaka 2017, jumla ya vijiji 4,000 zitakuwa vimepatiwa huduma hiyo.

Makama alisema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho kuzungumza na kampuni  ya simu kutoka Vietnam ijulikanayo kwa jina la Viettel na hivi karibuni wanatarajia kuzindua rasmi mpango huo.

Alisema kuwa kuna vijiji mbali mbali Tanzania havina kabisa mawasiliano na jukumu la serikali kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatatuliwa. 

Kwa mujibu wa Makamba sekta ya mawasiliano inazidi kukuwa na serikali imeweka mpango maalum kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma hiyo tena kwa ubora wa hali ya juu.

Alisema kuwa sekta hiyo ina changamoto nyingi kutokana na kupanuka kwa teknolojia ya mawasiliano na tayari serikali imechukua hatua kukabiliana na tatizo hilo hasa baada ya kukamilika kwa hatua ya tatu ya mkongo wa Taifa wa mawasiliano.
 
“Mpaka sasa ni mkoa wa Simiyu tu haujafikiwa na mkongo wa taifa na hiyo imetokana na kugawanywa kwa mkoa wa Shinyanga, hata hivyo mikakati inafanyika ili kuhakikisha mkoa huo unapata huduma hiyo na kuanza kufurahia huduma ya Tehama,” alisema Makamba.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte alisema kuwa anaamini kuwa kukamilika kwa mkongo wa Taifa kutanufaisisha nchi jirani ambazo hazina bahari.

Shamte ambaye kampuni yake ilidhamini mkutano wa mwaka 2012 alisema kuwa wanafuraha kubwa kuona nchi inafanya juhudi za kutatua tatizo la mawasiliano vijijini na nchi takribani nane zinazoizunguka Tanzania.
 
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alisema kampuni yao imeanzisha kitengo cha mtandao wa internet ambacho kitatoa huduma hiyo kwa bei nafuu.
 
“Lengo letu kubwa ni kurahisisha mawasiliano, hivyo tunawahikikishia kuwa watu wote wanaoishi vijijini watapata huduma hii kwa bei nafuu,”  alisema Ngota.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...