Skip to main content

WAZIRI MKUU AKARIBISHA WAWEKEZAJI WA POLAND


*Wengi wajitokeza katika sekta za kilimo, afya, madini, nishati na hoteli

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili nchini Poland kwa ziara ya siku mbili ya Kiserikali ambayo inalenga kuwavutia wafanyabiashara wa nchi hii waje kuwekeza Tanzania.



Mara baada ya kuwasili jijini Warsaw, akitokea London Uingereza, Waziri Mkuu jana jioni (Alhamisi, Oktoba 23, 2014) alikutana na wafanyabiashara zaidi ya 50 kwenye mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Chama cha Wafanyabiashara cha Poland (Polish Chamber of Commerce).


Katika Mkutano huo, Waziri Mkuu aliwaeleza mipango ya Serikali ya kuikwamua Tanzania kiuchumi huku akigusia sekta za kilimo, uvuvi, uchukuzi, miundombinu, madini, nishati na utalii.


“Nia ya ziara yangu fupi lakini yenye malengo mahsusi ni kuamsha mahusiano baina ya nchi zetu mbili lakini zaidi ni kutafuta mbinu za kukuza biashara kati ya Tanzania na Poland. Nataka muione Tanzania kama mahali salama pa kuwekeza mitaji yenu, mahali rafiki pa kuweka mitaji lakini pia mahali pa kufanya biashara ambayo pia itahusisha uwekezaji,” alisema.


Katika mkutano huo Waziri Mkuu alijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya 10 ambao walikuwa na shauku ya kutaka kufahamu ni maeneo yapi zaidi yanayohitaji uwekezaji.


Pia aliishukuru Serikali ya Poland kwa kusaidia ukarabati na uimarishaji wa miundombinu kwenye Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Tengeru, kilichopo Arusha.


Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kuongea na wafanyabiashara hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland anayeshughulikia masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati, Bibi Katarzyna Kacperczyk alisema nchi hiyo imeanzisha mpango maalum ujulikanao kama “Go Africa” ambao umelenga kukuza mahusiano ya kiuchumi na bara la Afrika.


“Tukiwa ndani ya Jumuiya ya Ulaya, pamoja na hatua kubwa za kiuchumi tunazokwenda nazo, kama Serikali tuliamua kwa dhati kwamba hatuwezi kuwaacha ndugu wetu wa iliyokuwa Ulaya Mashariki kabla ya mageuzi ya kiuchumi duniani... lakini tumeamua kuangalia bara la Afrika kama mdau muhimu wa maendeleo lakini pia kama soko la uhakika kwa bidhaa tunazozalisha,” alisema.


Alisema mpango huo umeanzisha mahsusi ili kuwasaidia wafantabiashara wa Poland kupata taarifa sahihi na haraka kuhusiana na masuala ya ushirikiano na uwekezaji barani humo.


Alisema wameanzisha mpango huo ili kuwahamasisha wenye makampuni barani Afrika waone kuna wenzao wa Poland na waamue kushirikiana katika kulijenga bara la Afrika.


Waziri Mkuu leo atatembelea kampuni ya Rol Brat inayotengeza zana za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na mashine za kuvuna mazao mazao mashambani. Pia atatembelea kampuni ya “Mtynpol” ambayo inahusika na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia vyakula na miundombinu yake.


Kesho asubuhi atakutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jijini Warsaw. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...