Skip to main content

WAZIRI MKUU AZINDUA JARIDA LA FIRST JIJINI LONDON


*Ni Toleo Maalum la Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania

*Linatumika kuitangaza Tanzania kwa watu mashuhuri


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua jarida la kimataifa la FIRST ambalo limesheheni taarifa za kuitangaza Tanzania kwa wadau wa nchi mbalimbali duniani huku likielezea hatua mbalimbali za ustawi kwa miaka 50 tangu nchi ipate uhuru.


Uzindusi huo ulifanyika kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza ambako pia Waziri Mkuu alikabidhiwa nakala ya kwanza ya toleo la sasa ambayo iliwekwa kwenye jalada jekundu la ngozi (leather bound red cover).


Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema Serikali ya Tanzania imepata fursa nzuri ya kujinadi kwa watu maarufu na wafanyabiashara wa kimataifa duniani kupitia jarida hilo na akataka uwekwe utaratibu wa kujinadi kisekta.


Alimtaka Balozi wa Uingereza, Bw. Peter Kallaghe aweke mkazo na kusimamia suala hilo ili kuhakikisha matoleo yanayofuata yanakuwa ya kisekta zaidi. “Balozi hapa umefanya kazi nzuri sana ya kuinadi nchi yetu, wala usichoke. Tujitahidi sasa kila mwaka waandike kuhusu fursa za uwekezaji kwa miradi ya kisekta kama utalii, nishati, madini na kadhalika,” alisema.






Waziri Mkuu alimshukuru Mwenyekiti wa taasisi ya First, Bw. Rupert Goodman kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa ajili ya Taifa la Tanzania. “Kazi uliyoifanya ni nzuri lakini katika tolea lijalo tuangalie jinsi ya kuitangaza miradi ya uwekezaji ambayo inauzika na iende sekta kwa sekta. Ukisirikiana na Balozo wetu hapa, lazima utapata kitu kizuri,” alisema.






Mapema, akielezea kuhusu jarida hilo la FIRST, Balozi Kallaghe alisema jarida hilo linasambazwa kwenye mashirika mbalimbali ya ndege kama vile British Airways, Air Astana, Lufthansa, United Airlines, Gulf Air, American Airlines, South African Airways, Korean Airways, Etihad Airways, Qatar Airways na Continental Airlines.






“Siyo tu kwamba linasambazwa katika mashirika haya ya ndege, bali pia linawekwa kwenye vyumba vya kupumzikia (First Class and Business Class Lounges) abiria wa daraja la kwanza na la pili wa mashirika haya kwenye viwanja vingi vya ndege,” alisema.




Alisema hili ni toleo la sita ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano na ofisi yake (Ubalozi wa Uingereza) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania lakini pia ikilenga kutangaza fursa za uwekezaji lakini pia ikitangaza hatua mbalimbali za maendeleo ambazo nchi hii imepitia.




Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Charles Kitwanga. Wengine ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu ambao pia wamefuatana na Waziri Mkuu.





IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 23, 2014

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...