Skip to main content

AZIMIO LA ARUSHA LA KUKABILI UJANGILI LAPITA




Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza kwenye mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu ulioshirikisha mataifa ya Afrika, wajumbe wa Bunge la Marekani (Congress) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mataifa washirika wa maendeleo, wanazuoni na wawakilishi wa taasisi zisizo za serikali uliomalizika jana jijini Arusha na kufungwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Kushoto Mwenyekiti wa mkutano wa kikanda wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha na kulia ni Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli.

Na mwandishi wetu, Arusha

JUMUIYA ya kimataifa imepitisha Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama.

Azimio hilo limepitishwa baada ya mkutano wa siku mbili ambapo pia imekubalika kwamba hali ya baadae ya wanyama barani Afrika ni suala linalohitaji uwajibikaji wa pamoja.

Aidha nchi za Afrika zimetakiwa kuukomesha ujangili na kufanya juhudi ya kuhakikisha wanyama walio katika hatari ya kutoweka wanalindwa na kuhakikisha kundi hilo linakua.

Wanyamama ambao kwa sasa wapo hatarini kutoweka ni tembo, faru na simba.

Mkutano huo uliojumuisha mataifa mbalimbali ya Afrika na jumuiya za kimataifa na kufunguliwa na Waziri wa Mali asili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwa niaba ya rais Jakaya Kikwete, umetoa wito kwa mataifa yote kufanyakazi kwa pamoja kukabili ujangili kwa kushirikisha wananchi wanaoishi na kutegemea wanyamapori hao na mapori yenyewe.


Washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu wakijadilina namna ya kuweka nguvu ya pamoja katika kukabiliana na suala la ujangili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu, baada ya mkutano ambao uliangalia sheria zilizopo za kulinda mapori na wanyamapori,uhalisia wa mifumo ya ujangili na uhifadhi, washirika wa maendeleo nao walielezea nia zao za kuendelea kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na mapori katika ukanda wa Afrika ikiwamo Tanzania.

Mkutano huo ambao ulishirikisha mataifa ya Afrika, wajumbe wa Bunge la Marekani (Congress) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mataifa washirika wa maendeleo, wanazuoni na wawakilishi wa taasisi zisizo za serikali umeelezwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya London, Uingereza ya kustawisha wanyamapori na mapori yanayowahifadhi.

Awali akifungua mkutano kwa niaba ya Rais Kikwete, Waziri Nyalandu alisema kwamba mataifa yasidharau nguvu ya pamoja katika kukabiliana na ujangili.

Alisema pia kwamba hali ya baadae ya wanyamapori katika bara la Afrika ni wajibu wa kila mtu na kila taifa na mamlaka nyingine ambazo ni wadau.


Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ambapo amesema UN itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mamlaka mbalimbali zinazoendelea kukabiliana na ujangili na kupotea kwa misitu duniani ili kuhifadhi urithi wa dunia.

Alisema Tanzania katika mchango wake imeanzisha mkakati wa kukabiliana na ujangili na kuunda mamlaka ya wanyamapori ili kuwa na uhakika wa kuendeleza masuala yanayohusu hifadhi na changamoto zake kwa kasi na karibu zaidi.

Washiriki wa mkutano huo wa siku mbili walielezea umuhimu wa kulinda mali asili hizo kwa kuwa ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi zote.

Akizungumzia umuhimu wa mali asili Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, alisema ujangili na uhalifu mwingine kwa wanyamapori na hifadhi zao ni changamoto kubwa kwa uchumi unaotegemea utalii, mazingira na maendeleo endelevu.

Alisisitiza kwamba suala la uhalifu kwa wanyamapori na mapori yao ni lazima kufanyiwa kazi kitaifa na kimataifa ikiwamo kikanda.

Mratibu huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia juhudi hizo za kuhifadhi wanyama na mapori kwa kusaidia kutoa elimu na kutatua changamoto za kiuchumi zinazokabili watu wanaoishi jirani na misitu hiyo.


Pichani juu na chini ni washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu uliomalizika jana jijini Arusha.

Alisema Umoja huo utaendelea kusaidia kupeleka elimu ya menejimenti ya wanyamapori na misitu ili wakazi wa maeneo hayo wafaidi raslimali hizo na kuzitunza.

Hata hivyo alizitaka jumuiya za kimataifa na mataifa kushirikiana katika kufanikisha adhma hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya ICCF ambao ni wenyeji wenza wa mkutano huo, Makamu Mwenyekiti Dk Kaush Arha, alisema mkutano huo ulikuwa na manufaa makubwa hasa wito wa kuweka mikakati ya kurejesha makundi ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka kama tembo, faru na simba.

Aidha mkutano umekubaliana juu ya masuala kadhaa ambayo yatasaidia Tanzania kuingia makubaliano na majirani zake kuhifadhi wanyamapori.


Naye Mkuu wa balozi za nchi za Jumuiya ya Ulaya nchini Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyochukua kukabiliana na ujangili.

Amesema Jumuiya ya Ulaya ambayo imekuwa mshirika katika kukabilina na ujangili na hifadhi ya wanyama imefurahishwa na mkutano huo kwa kuamini kwamba kunatakiwa kuchukuliwa hatua za kikanda kuweza kunusuru wanyamapori kwa kuchukua hatua za pamoja.

Ameipongeza Tanzania na majirani zake kwa kuchukua hatua madhubuti za kikanda kukabiliana na ujangili na uharibifu wa mazingira na kusema Jumuiya ya Ulaya ipo tayari kusaidia katika juhudi hizo.



Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia utiliwaji saini wa Azimio hilo.


Wawakilishi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kenya, Malawi, Uganda, Mozambique, Tanzania, na Zambia wakisaini Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama kabla ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa tatu kushoto) kufunga rasmi mkutano huo uliomalizika jana jijini Arusha.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...