Skip to main content

MFUKO WA GEPF WAPANUA WIGO KWA KUZINDUA OFISI MPYA NYANDA ZA JUU KUSINI

 Meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini Bw Ramadhan Sosora akitoa neno la ufunguzi na utambulisho kwa wanahabari.
 Meneja Masoko kutoka Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF Bw Aloyce Ntukamazina akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo kulia kwake ni Afisa masoko katika ofisi ya mbeya Bw Alex William.

 Pichani baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo wakati wa uzinduzi huo.

Bw Aloyce Ntukamazina akielezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 toka 2004 – 2014 yaliyopelekea uzinduzi wa ofisi mpya nyanda za juu kusini.

 Uongozi wa Mfuko wa GEPF ukipokea maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari juu ya mipango ya Mfuko wa GEPF katika kupanua wigo zaidi na kufikia watanzania walio wengi.


Baadhi ya waandishi wa habari walioalikwa wakichukua picha za tukio hilo katika ukumbi wa mikutano wa Mfuko wa GEPF.



Bw Aloyce Ntukamazina Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF alielezea kuwa sababu kubwa zilipelekea kuzindua ofisi mpya nyanda za juu kusini kwanza ni ukuaji wa kasi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara katika mkoa wa Mbeya lakini pia ni mafanikio makubwa ambayo Mfuko umeyapata kwa kipindi cha miaka 10 kutoka 2004 ambapo mfuko ulipata menejimenti yake rasmi hadi 2014.

Alisema Mfuko umekuwa katika vigezo vyote kwa upande wa wanachama wameongezeka kutoka 16,131 hadi kufikia 76,000, Michango imeongezeka kutoka TZS 5.1 Billioni kwa mwaka hadi TZS 37.29 Billioni na Thamani ya Mfuko imeongezeka kutoka TZS 20.21 Billioni 2004 hadi TZS 245.38 Billioni 2014.

Ukuaji huu umeonyesha Mfuko una afya njema na unaweza sasa
kupanua wigo na kufungua ofisi mpya katika mikoa mingine. Jambo la pili Bw Ntukamazina alieleza ni ukuaji wa kasi wa mpango wa hiari wa VSRS ambao kwa kipindi kifupi cha miaka mine tangu uanzishwe 2010 umeweza kuwasajili jumla ya wajasiriamali 35,481 ambao kwa kipindi kifupi hicho wamejiwekea akiba ya zaidi ya TZS 5.01 Billioni. Alisema hii imedhihirisha
kwamba mpango huu ni mkombozi kwa watanzania wote na Mfuko ukaona ni vyema sasa usogeze huduma zake karibu kwa watanzania waishio nyanda za juu kusini ili naoNwaweze kufaidika na mafao yatolewayo.

Mwisho Bw Ntukamazina alitoa wito kwa watanzania wote wajengeutamaduni wa kujiwekea akiba kwani uzee hauepukiki na ipo siku kila mmoja wetu
ataishiwa nguvu za kuzalisha mali, lakini pia alisema GEPF kupitia mpango wa NVSRS ina mipango madhubuti kuhakikisha kila mtanzania awe mkulima, mama lishe,mjasiriamali, muuza mitumba, mvuvi n.k nao wanalipwa Pensheni kama wengine walio
katika ajira rasmi.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...