Skip to main content

PINDA ATAKA VITA DHIDI YA UJANGILI IWE YA PAMOJA


IMG_5158
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga Mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu na wa pili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

* Ataka iundwe timu kufuatilia utekelezaji wa Azimio la Arusha 2014

Na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwa wadau wote katika kutekeleza Azimio la Arusha la kukabiliana na ujangili na kuendeleza hifadhi za wanyama katika nchi za Afrika Mashariki na zilizo Kusini mwa Ikweta.


Akizungumza na waandishi wa habari juzi mara baada ya kufunga mkutano wa kikanda wa siku mbili uliojadili mbinu za kupambana na biashara haramu ya wanyamapori ulioandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha, Waziri Mkuu alisema: “Suala hili linataka uwajibikaji wa pamoja. Mashirika na taasisi, wananchi na viongozi sote kama wadau wakuu, kila mmoja anapaswa kushiriki vita hii kama kweli tunataka tuitokomeze.”

“Kwenye hili Azimio la Arusha na nyie waaandishi wa habari pia mna sehemu yenu mmetajwa... wamesema wanatafuta jinsi ya kushirikiana na vyombo vya habari ili visaidie kutoa elimu kwa jamii kama njia ya kuelimisha umma,” alisema.

Waziri Mkuu aliwaeleza waandishi hao kwamba Azimio hilo lina vipengele 20 ambavyo vinataka utekelezaji katika ngazi ya nchi mojamoja, ngazi na kanda na ngazi ya kimataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

IMG_5160
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akielekea kwenye chumba cha mapumziko kabla ya kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.

“Nimepata faraja kwamba mkutano huu haukuisha kijumlajumla tu, bali umekuja na maazimio 20 ambayo yametengwa kwa ajili yetu sisi wa ndani, mengine yanahusisha ushirikiano wa kikanda na yako mengine yanawahusisha wadau wa maendeleo,” alifafanua.

Ili kutekeleza azimio hili, nimeshauri iundwe timu itakayoshirikisha vyombo vingi zaidi badala ya kuiachia Wizara ya Maliasili na Utalii peke yake. Timu hii ikutane kila baada ya miezi sita ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio haya na ikibidi Waziri atoe taarifa bungeni kuhusu utekelezaji huo,” alisema Waziri Mkuu.

Mapema, akizungumza na washiriki wa mkutano huo wakati wa kuufunga, Waziri Mkuu alisema kuwepo kwa watu wa ngazi tofauti kwenye mkutano huo ni kielelezo tosha cha umakini wao na nia thabiti ya kutokomeza ujangili katika ukanda huu.

IMG_5167
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.


“Tumeanzisha vita, tusisahau kwamba bado kuna kazi kubwa mbele yetu na vita haijaisha. Tuzidishe mapambano katika sehemu tatu: kwenye nchi unakofanyika ujangili, nchi ambazo nyara zinapitishwa na nchi zinazopokea ama kununua hizo nyara,” alisema Waziri Mkuu.

“Nakubaliana nanyi kwamba hakuna nchi inayoweza kukabili suala la ujangili ikiwa peke yake. Tunahitaji tuwe na sera mahsusi, sera ya pamoja ya kutuunganisha na kutuongoza wakati tukitekeleza Azimio hili kwa kusaidiana na wadau wa maendeleo,” alisema.

Alisema Azimio hilo litaipa kazi ya ziada ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo kazi kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa wa Azimio hilo unakuwa wa ufanisi.
Jumla ya nchi tisa zimetia saini azimio hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.

IMG_5170
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, huku Waziri wa Mali asili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akifurahi jambo ndani ya chumba cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye chumba cha mikutano.

IMG_5169
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli (wa pili kulia) kwenye chumba cha mapumziko baada ya kuwasili ukumbi hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.

IMG_5182
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye chumba maalum cha mapumziko.

IMG_5253
Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kushoto) kufunga rasmi mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Magese Mulongo, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli wakiwa meza kuu.

IMG_5264
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza na wadau waliohudhuria mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014 wakati akifunga rasmi mkutano huo wa siku mbili.

IMG_5198
Mwakilishi wa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania akichukua taswira za baadhi ya matukio yaliyokuwa yakiendelea mkutanoni hapo.

IMG_5197
Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo.

IMG_5236
Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi tisa wakitia saini Azimio la Arusha la kukabili ujangili mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.

IMG_5205
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwenye ufungaji wa mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.

IMG_5224
Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke, akizungumza kwa niaba ya serikali ya Ujerumani.

IMG_5212
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu wakati wa ufungaji rasmi wa mkutano huo uliodumu siku mbili jijini Arusha.
IMG_5268
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka ukumbini hapo mara baada ya kuufunga rasmi mkutano huo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...