Skip to main content

RC IRINGA AKABIDHI MIFUKO YA SARAJI 115 KWA MANISPAA YA IRINGA




Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma (wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Leticia Warioba jana kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 115 ya sementi yenye thamani 1,725,000/- kwa ajili ya  ujenzi wa maabara katika shule za sekondari. Wanaoshuhidia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Ayub Wamoja (kulia) na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma jana amekabidhi msaada wa mifuko 115 ya sementi yenye thamani 1,725,000/-kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo kwa ajili ya  ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.


Dkt. Ishengoma kwa kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa ametoa mifuko  ya sementi hiyo ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara na kuwataka wananchi na taasisi mbalimbali kujitolea kuchangia ujenzi huo ili kuongeza kasi ya kuzalisha walimu wa masomo ya sayansi.

Alisema kuwa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari ni utekelezaji wa agizo la rais aliyezitaka shule zote za sekondari nchini kuwa na maabara tatu kwa kila shule.

Akipokea msaada huo wa vifaa vya ujenzi mkuu wa wilaya iringa, Leticia Warioba kwa niaba Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo aliwaomba wadau mbalimbali yakiwemo mashirika, taasisi, watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kujitokeza kuchangia ujenzi wa maabara.

Warioba alisema kuwa ili kufanikisha malengo ya wilaya ya iringa inahitaji michango ya wadau mbalimbali  ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyezitaka halmashauri zote kuhakikisha zinajenga  maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema manispaa hiyo inahitaji maabara za kudumu 28 na hadi sasa kuna jumla ya maabara 22 zinaendelea kujengwa na maabara sita ziko katika hatua ya mwisho kukamilika.


Hata hivyo, maabara zinazoendelea kujengwa katika manispaa hiyo ni pamoja na vyumba vya maabara ya fizikia, kemia na baiolojia ifikapo mwaka 2016. 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...