Skip to main content

Watahiniwa 11,781 mtihani wa kidato cha nne kufanya mtihani mkoa wa Iringa

afisa_elimu_b3ba5.jpg

Ofisa Elimu Mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwaka. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Na Friday Simbaya, Iringa

MITIHANI ya wanafunzi wa kidato cha nne na maarifa (Qualifying Test) kitaifa unatarajia kufanya nchini kote hapo tarehe 3 Novemba mwaka huu.


Mkoa wa Iringa unatarajia kuwa na jumla ya watahiniwa 11,781 watakaofanya mtihani wa kidato cha nne na mtihani wa QT taifa na kuaswa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ambavyo vitakavyowaondolea sifa ya kuendelea kufanya mitihani yao.

Rai hiyo imetolewa na Ofisa Elimu Mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi jana wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Ofisa Elimu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa watahiniwa wanatakiwa kujiepusha na vitendo vyote vya udanganyifu ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye vyumba vya mitihani na karatasi za majibu na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutawaondolea sifa ya kuendelea mitihani yao.

“Nikiwa kama ofisa elimu mkoa wa Iringa nimeagiza watahiniwa wote kuzingatia maelekezo ya wasimamizi wa mitihani na wasimamizi nao wazigantie maelekezo ya semina ya maelekezo kwa wasimamizi,” alisema ofisa huyo.


Alisema kuwa mkoa wa Iringa utakuwa na jumla ya vituo vya kufanyia mitihani 186 na vitasimamiwa na wasimamizi 408 ambapo, wasimamizi wakuu watakuwa 46 pamoja na walimu 309  watakaosimamia mitihani ya vitendo (practical tests).

Aidha, ofisa huyo alisema kuwa kwa mwaka jana Mkoa wa Iringa ulivuka lengo la ufaulu ya matokeo makubwa sasa (BRN) ya asilimia 60 kwa kufaulisha wanafunzi zaidi kwa asimilia 64.92 na kuongeza kuwa mwaka lengo ni asilimia 70.

Hivyo aliwataka watahiniwa wote wanaotarajia kufanya mitihani hiyo, kujiamini kwa vile katika kipindi cha muda wa miaka minne waliyokuwa shuleni wamejifunza mambo yote ya msingi watakayofanyia mihitani hiyo.



Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...