Skip to main content

ZAIDI ya walinzi 60 wa Kampuni ya Kiwango Security Guards Ltd wagoma tena...!

Katibu Mkuu wa TUPSE, Edison Kivelege akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Baadhi wa walinzi wakiwa mabegi ofisini kwa TUPSE


ZAIDI ya walinzi 60 wa Kampuni ya Kiwango Security Guards Ltd kanda ya Iringa kwa mara nyingine wamegoma kuendelea na kazi ya kulinda minara ya Vodacom/Tigo wakidai mishahara ya miezi mitatu.


Walinzi hao kutoka sehemu mbalimbali ya mkoa wa Iringa wakiongea na SIMBAYABLOG leo kwa machungu katika ofisi za Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE), Kanda Nyanda za juu Kusini zilizopo mjini Iringa, walisema kuwa wana muomba Rais Jakaya Kikwete aingilie kati katika mgogoro wa mwajiri wao ili awalipe mishahara yao ya miezi mitatu wanayomdai.

"Mwajiri huyo ni wa kampuni ya ulinzi ya kiwango kutoka jijini Dar es salaam hajatulipa mishahara yetu, kwa kweli hali ni nguu kweli sasa sisi tunafanya kazi kama nyuki tunatumikishwa na hadi sasa tuna miezi mitatu na zaidi hatujalipwa na hatujui familia zetu zinaishi vipi huko nyuma, hivyo tunamuomba rais aingilie kati suala hili ilituwezekulipwa mishahara yetu.'walisema.


Mzee Ismaili Mpenge (68) ambaye analinda mnara wa Vodacom kadeti uliopo kijiji cha Nyang'oro katika jimbo la isimani Iringa alisema kampuni hiyo haijamlipa mishahara ya miezi miwili tangu aanze kazi Julai nne mwaka huu.

Alisema kuwa tangu jana afike mjini iringa kutoka kijijini kwake hajala na nauli yakufika mjini amekopa na kuongeza kuwa hapa mjini hana ndugu na kuomba wasamaria wema wamsaidie sehemu ya kulala anaposubiria malipo.

"Nimetoka katika kijiji cha Nyang'oro tangu jana na sijui hatma na isitoshe tuna watoto wanasoma na mpaka sasa hatujui familia zetu zinakula nini mpaka sasa ... kwa kweli maisha yetu walinzi ni magumu," alisema.

Naye Isaya Mdabagi mlinzi wa mnara wa migori alisema kuwa kwa miezi miwili hatujalipwa mishahara ukizingatia tuna familia tulizoziacha huku nyumbani bila chochote.

Mwajiri aliahidi kulipa mshahara wa mwezi moja na sio mshahara wote kama makubaliano yetu ya kulipwa laki na ishirini lakini amesema kuwa watalipwa shilingi elfu themanini .

Hata hivyo, kuna baadhi ya walinzi ambao waliokosa hela  ya kulala gesti waliamua kulala ofisiza TUPSE kwa kukosa ndugu hapa mjini.


Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa TUPSE, Edison Kivelege aliongeza kuwa Iringa ina jumla ya makampuni ya ulinzi binafsi 36 nyingi zikitoka nje ya mkoa, lakini pamoja na hayo kampuni zenye ofisi azizidi kumi (10) na kusababisha kukosa mawasiliano.


Alisema kuwa chama kinapotaka kuwasiliana na wanachama wake kinapata shida ya kuonana na viongozi kwa ajili yakutatua kero za wanachama kwa sababu ofisi nyingi za waajiri zipo Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam.


Alisema kuwa kampuni nyingi hapa Iringa zinafanyakazi za udalali kwa sababu hiyo kampuni hizo zinakuwa zinawaajiri walinzi wasiokidhi vigezo ambao wanakuwa na uweledi mdogo kuhusiana na masuala ya ulinzi na wengine kuajiriwa bila mikataba maalum.

Katibu Mkuu wa TUPSE huyo aliwaasa walinzi kuacha tabia ya kuhamahama makampuni kwa sababu wanajisababishia kupoteza mafao na uaminifu na kuwahimiza wajisajili na chama hicho ili washiriki katika mabaraza ya majadiliano na waajiri.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...