Skip to main content

MAMA KIKWETE AWATAKA VIJANA KUWA NA MSIMAMO NA KUTOKUBALI KUTUMIKA KATIKA VURUGU




Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka vijana kuwa na msimamo na kutokubali kutumika katika vurugu zinazohatarisha amani na usalama wa nchi.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati akifungua shina la vijana wakeleketwa la kikundi cha Zahanati Kempu lililopo Kata ya Rasibura wilaya ya Lindi mjini.


Alisema vijana wengi hawajui Historia ya nchi hivyo basi baadhi ya watu wasio na nia njema wanaitumia nafasi hiyo kuwarubuni na kuwashawishi kufanya vurugu zinarudisha nyuma maendeleo ya eneo husika.

“Msikubali mkoa wetu wa Lindi kuwa kichaka cha majaribio na kutumika katika vurugu, kuweni na msimamo wa kuitetea amani yetu kwani mkifanya vurugu matatizo yanapotokea ninyi ndiyo mnaoangamia na hao waliowashawishi wanawakimbia”.

Kama atakuja mtu hapa na kuwashawishi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni sawa hakuna atakayezuia tunahitaji kuwa na maendeleo katika mkoa wetu, lakini kuwashawishi ili mfanye vurugu na kuharibu vichache tulivyonavyo msikubali”, alisema Mama Kikwete.

Aidha MNEC huyo aliwasisitiza vijana kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili waweze kujiletea maendeleo yao na ya mkoa huo kwa kuwa vijana ndiyo wanaotegemewa na ni nguvu kazi ya Taifa.

Akisoma taarifa ya kikundi hicho Hidaya Chivii ambaye ni Mtunza fedha alisema kikundi hicho kilianzishwa tarehe 5/7/2014 kikiwa na wanachama 23 kati ya hao wanaume ni 18 na wanawake ni watano.

Chivii alisema madhumuni ya kuanzishwa kwa kikundi hicho ambacho kinajihusisha na kazi ya kuendesha pikipiki (bodoboda) kwa upande wa wanaume na ususi kwa upande wa wanawake ni kujikwamua na hali ngumu ya maisha na kuweza kujiendeleza.

“Waendesha pikipiki tunakabiliwa na changamoto ya kunyang’anywa pikipiki hasa ifikapo wakati wa uchaguzi kwani wamiliki walio wengi ni wanachama wa chama cha Wananchi (CUF) na sisi ni wanachama wa CCM au wanatupa pikipiki zao kwa masharti magumu yakiwemo ya kukipigia kura chama chao”, alisema Chivii.

Alizitaja changamoto nyingine zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwa na vitendea kazi vyao wenyewe na kutokupata mafunzo ya ujasiriamali.

Wakati huo huo Mama Kikwete alifanya vikao na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM katika matawi ya Kilimahewa na barabara ya Kawawa na kuwahimiza wajumbe kuendelea kushikamana na kuwa kitu kimoja ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Akiwa katika tawi la Kilimahewa lililopo Kata ya Mwenge aliwapokea vijana wanne kutoka chama cha Wananchi (CUF) ambao walijiunga na CCM.

Mama Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini yupo wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi na kuangalia utekelezaji w

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...