Skip to main content

Mtaturu: Huwezi kumsafisha mtu wakati mikono yako ni michafu Na Mathias Canal, Mufindi


Mataturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano.

Mataturu (kulia akiwanadi wagombea uenyeviti wa mitaa kwenye mkutano uliofanyika mtaa wa Kinyanambo)

Na Mathias Canal, Mufindi
Wakazi wa Mtaa wa Kinyanambo, Kata ya Kinyanambo, Wilayani Mufindi wameaswa kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao ili kukabiliana na mabadiliko ya kujitegemea kwa Mamlaka ya mji wa Mafinga.

Akihutubia wananchi waliojitokeza Katika Mtaa wa Kinyanambo, mkutano huo wa kampeni kwa ajili ya viongozi wa serikali za Mitaa, Vitingoji na Vijiji ambapo uchaguzi unatarajia kufanyika Disemba 14, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alisema kuwa wananchi wanapaswa kuchagua viongozi watakaowatumikia kwa ufanisi na uwezo mkubwa kwa miaka mitano ijayo.
Alisema kuchagua viongozi wa vyama vya upinzani ni kufunga shughuli za maendeleo hivyo ni vyema kuchagua CCM ili kuendelea kukamilisha ahadi na ilani ya chama hicho.
"Ni bora kuwa mchawi kuliko mnafiki, mimi nawahakikishia kuwa vyama vya upinzani ni maalumu kwa ajili ya kuvuna pesa za wananchi( SACCOS) sio kwa ajili ya maendeleo yao" Alisema Mtaturu
Mtaturu alisema watanzania wanapaswa kutambua kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji ni muhimu kwa kuwa viongozi hao ndio wachapaji kazi za wananchi na wanatekelezaji kazi za wananchi kwa ufasahasa katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Kuna msemo waswahili wanasema usione vyaelea ujue.....wananchi wakaitikia VIMEUNDWA, basi kama mnalijua hilo msidanganywe na vyama vya msimu ambavyo havijui kwamba sisi tunatekeleza ilani ya chama na safari hii tumeianza muda mrefu hivyo abiria anayepandia njiani hawezi kujua nauli ya mwanzo wa safari" Alisema Mtaturu
Alisema kuwa Hakuna binadamu anayeweza kumsafisha binadamu mwenzake wakati mikono yake ni michafu, hivyo vyama vya upinzani vimekuwa vikiikosoa sana serikali kwa kila jambo inalolifanya pasipo kujali kuwa ni baya au zuri wakati vyama hivyo havina jambo lolote la kujivunia kwa maendeleo ya watanzania zaidi ya maandamano na vurugu ambazo zimesababisha wananchi wengi kupata ulemavu na wengine kupoteza maisha.
Mtaturu alitumia nafasi hiyo pia kuwanadi wagombea wote wanaowania nafasi za uongozi katika Mitaa mbalimbali ambapo wananchi walionekana kuitikia kwa wingi kufurahia wagombea wanaowania nafasi hizo jambo ambalo CCM imeona kuwa linaendelea kujenga imani ya chama hicho kwa wakazi wa Kinyanambo na Taifa kwa ujumla.
Alisema CCM ina amini katika misingi ya uvumilivu, heshima na nidhamu ndio maana hata wabunge wake huchangia hoja mbalimbali bungeni pasipo jazba na hasira badala yake hutumia hekima na ustaarabu wakiamini kwamba wananchi wanawasikia kwa kila jambo wanalolifanya.
Aidha alisema kuwa CCM ni chama kisichochagua wananchi wa kuwatumikia bali huwapa nafasi wananchi wake kuchagua viongozi wao wanaowataka katika ngazi mbalimbali kwani kufanya hivyo ni kutenganisha uongo na ukweli ambao wananchi wengi wanahitaji kufahamu.

  • Write a comment...

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...