Skip to main content

SALAMU ZA MKUU WA MKOA WA IRINGA ZA KUWATAKIA HERI WANANCHI WA MKOA WA IRINGA KATIKA SHEREHE ZA NOELI NA MWAKA MPYA 2015


Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Iringa
Ninayo heshima kubwa kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha tuwe na afya njema tokea tulipoanza mwaka 2014. Ni matumaini yangu kuwa Mungu atatuwezesha pia kuumaliza salama mwaka 2014 na hatimae kuuanza mwaka 2015.

Aidha, napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wananchi wote wa Mkoa wa Iringa kwa ushiriki wenu katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Ndugu Wananchi,
Katika kipindi chote cha mwaka 2014 wananchi wa Mkoa wa Iringa mmekuwa mkifanya kazi kwa kujituma na kwa ushirikiano mkubwa. Ni matumaini yangu kwamba tabia hii ya kufanya kazi kwa kujituma na mshikamano itaendelea Mwaka 2015.  Kufanya kazi kwa kujituma na mshikamano kutaleta tija na maendelo ya mwananchi mmoja mmoja na Mkoa wa Iringa kwa ujumla.

Ndugu wananchi;
Msimu wa kilimo tayari umeanza. Nitoe wito kwenu kuzitumia vizuri mvua zinazo endelea kunyesha. Muda huu ni muda muafaka wa kupanda mazao ili kujihakikishia uhakika wa chakula.

Katika maeneo yenye uzoefu wa kupata mvua chache hususani Mahenge, Isimani, pandeni mazao yanayovumilia ukame.  Aidha, tukumbuke kupanda miti katika Msimu huu wa mvua kwa kuwa Mkoa wetu unahali ya hewa nzuri inayostawisha miti.

Ndugu wananchi;
Tunapopanda mazao mbalimbali tumieni mbegu bora, mbolea ya kupandia na kukuzia hasa kwa kilimo cha Mahindi na Mpunga ili kupata mazao bora. Wahenga walinena kuwa “Mvua ya kwanza ni mvua ya kupandia”

Ndugu Wananchi; Ulinzi na Usalama
Nawaomba sana ndugu zangu wananchi wa Mkoa wa Iringa, kwa umoja wetu tuhakikishe tunasimamia na kudumisha Ulinzi na Usalama ili Mkoa wetu uendelee kuwa na amani na utulivu. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunatokomeza kabisa vitendo vyote vinavyopelekea uvunjifu wa amani katika Mkoa wetu wa Iringa na nchi yetu kwa ujumla. Sote tujikite kwenye shughuli za maendeleo na kudumisha umoja.  Hali ya usalama ya Mkoa ni shwari na Vyombo vyote vya Dola vitaendelea kuwa makini katika kusimamia amani na utulivu katika Mkoa wa Iringa ili wananchi waweze kushiriki katika shughuli zao za kujiletea maendeleo.

Salamu za Noeli na Mwaka Mpya 2015
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwatakia sikukuu njema ya Noeli na Mwaka Mpya 2015 wenye mafanikio tele. Ninawasihi kuhakikisha mnasherehekea sikukuu hizi kwa amani, usalama na utulivu.

Serikali itahakikisha ulinzi na usalama vinakuwepo kipindi chote cha sikukuu kwa sababu uzoefu unaonesha kuwa katika majira ya sikukuu watu wasiopenda kuona amani na utulivu wa Mkoa hutumia majira haya kufanya uhalifu.  Ulinzi uanzie ngazi ya kaya, kila mwanafamilia awe makini na kutoa taarifa anapokuwa na wasiwasi na jambo linaloweza kuhatarisha amani na usalama wake na wa Mkoa kwa ujumla.

Wazazi, kipindi hiki cha Sikukuu ni kipindi muafaka cha kukaa na familia kutafakari tulikotoka, tulipo na tunapokwenda. Ni wakati muafaka wa kupanga malengo ya familia na namna ya kuyafikia.

Mwisho,
Mvua zinaendelea kunyesha zimeanza kusababisha maafa, hivyo nawasihi wananchi wote kuchukua tahadhari, hususani wanaoishi mabondeni naomba wahame maeneo hayo.

Ndugu wananchi,
Baada ya kusema haya asanteni kwa kunisikiliza na nawatakia Sikukuu njema ya Chrismas na Mwaka Mpya (2015).

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...