Skip to main content

WENYEVITI NA WAJUMBE WA KAMATI SERIKALI ZA MITAA WAAPISHWA...!


Wakili wa kujitegemea Charles Paul Lawisso akiwaapisha wenyeviti na wajumbe kamati za mitaa manispaa ya iringa katika ukumbi wa orofea.



 Kaimu  mkurugenzi wa manispaa ya iringa Augustno Nyenza


wajumbe wakisaidiana kujaza fomu za kiapo ndani ya ukumbi




WENYEVITI wa serikali za mitaa walichaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika manispaa ya iringa wameapishwa jana kwa kupewa onyo kali na wakili wa kujitegemea Charles Pau Lawisso kwamba atakayeenda kinyume atachukuliwa hatua kali za kisheria.


 Lawisso ambae ni wakili wa kujitegemea alitoa onyo hilo wakati wenyeviti hao    wakiapishwa mjini iringa.

  “Wapo viongozi watakaosema sera ya chama chetu hairuhusu wananchi kuchangia miradi ya maendeleo na ama wapo watakaozuia michango kwa lengo la kulinda na kutetea wapiga kura wao…kitendo hicho kitakiwa kinakwenda kinyume na sheria za nchi na hivyo ukibainika hatua zitachukuliwa dhidi yako.”alisema lawisso.

 Aliongeza kuwa kazi za wenyeviti hao kuwa ni pamoja na kufuatilia miradi ya maendeleo katika mtaa husika na kutekeleza maagizo kutoka ngazi za juu yaani kata na Manispaa.

Lawisso wakati akitoa onyo hilo limekuja sera ya chadema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa ni kuhakikisha inazuia michango isiyoyalazima kwa wananchi wake, kutochangisha michango kwa ajili ya huduma za kijamii ikiwamo utoaji wa barua za dhamana na mikopo kutoka katikataasisi mbalimbali.

Pia alitaja kazi za wenyeviti hao kuwa pamoja na kufuatilia na kusimamia miradi ya maendeleo watakuwa na jukumu la kusuluhisha migogoro inayotokea katika mitaa yao ambayo maamuzi yake hayahitaji kufika ngazi za juu.

Nae kaimu  mkurugenzi wa manispaa ya iringa Augustno Nyenza alisema kuanzia sasa wenyeviti na wajumbe waliochaguliwa na viongozi wa serikali watakaosaidia na ofisi yake kutekeleza masuala ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Leo mmeapa kulitumikia taifa na wananchi kwa ujumla na baada ya kiapo hiki mnapaswa kutambua kuwa kazi mmeanza rasmi na leo hii mmekuwa viongozi wa kamili wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,mtafanya kazi zenu kwa kushirikiana na watendaji wa serikali za mitaa,kata na Halimashauri ya manispaa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku”alisema Nyenza.

Katika uchaguzi huo uliofanyika hivi karibuni jumla ya wenyeviti 192 wa manispaa ya iringa na wajumbe 960 walitarajia kula kiapo cha utii kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mitaa yao.

Uchaguzi huo uliofanyika ni kwamba jumla ya 192 huku chama cha mapinduzi CCM kikijinyakulia viti 126 na chadema 64 na CUF viti viwili.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...