Skip to main content

WWF YAMWAGA VIFAA VYA BUSTANI KWA SHULE ZA MUFINDI

 Wanafunzi wa shule ya msingi igomaa wilaya ya mufindi wakipata maelekezo ya namna ya kuanzisha vitalu cha bustani ya miti kutoka mtaalam.


Ofisa Maendeleo ya jamii msaidizi, martha Sanga vifaa ya bustani mwalimu wa shule ya sekondari sadani.




Wanafunzi wa shule ya msingi igomaa walifurahia kamera.





Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) kupitia Programu ya Maji Ruaha (RWP), mkoani Iringa limekabidhi vifaa kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya bustani za miti katika shule mbalimbali za Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.



Ofisa Maendeleo ya Jamii msaidizi wa shirika hilo, Martha Sanga alisema vifaa vilivyotolewa ni pamoja na tolori,water can,leki, viliba, majembe, chepe na mbegu aina saba za miti, ambavyo vilikabidhiwa kwa kamati za mazingira za shule.

Shule zilizopewa nyenzo hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Sadani, Shule ya Msingi ya Igomaa na Shule ya Sekondari Isalavanu.

Alisema kuwa zaidi ya shilingi milioni tatu (3m/-) zilitumika kwa ajili ya vifaa pamoja na malipo ya wawezeshaji, mafuta ya gari na mengineyo.

Alisema kuwa wameamua kutoa vifaa hivyo kwa shule ilikupandiza mbegu ya uhifadhi kwa watoto wa shule na hatimaye kupeleka elimu ya kutunza mazingira kwenye familia zao. na imeshindwa kutunza miti ya matunda katika mashamba darasa hayo zilizotolewa na shirika hilo.

“Tuliwahi kuipa jamii mbegu za miti ya matunda iliweze kuanzisha bustani za matunda wakashindwa kuitunza na kwa safari hii tumeamua kuwapa wanafunzi vifaa vya bustani kupitia kamati zao za mazingira kwa sababu ni rahisi kutunza mazingira,” alisema Sanga.

Naye mtaalamu kutoka idara ya ardhi na maliasili kitengo cha misitu, Khalid Kayowa wa halmashauri ya wilaya Mufindi alitoa mafunzo kwa kamati za mazingira hizo ya namna ya kutumia vifaa pamoja na namna ya kutungeza vitalu vya miche.

Alivitaja vitu vinavyohitajika kuanzisha eneo la kuwatika mbegu za miti kuwa ni udongo,mchanga, mbolea ya mbonji pamoja na viliba na madawa kwa ajili ya kuulia wadudu na lazima na kivuli cha kutosha pamoja kuwe na uzio.

Alisema kuwa kamati za mazingira hizo hazinabudi ya kufuata ushauri wa kitaalamu ya namna ya kuanzisha bustani kwa ajili ya kuzalishia miche ya miti itakayopandwa katika maeneo mbalimbali shule.

Shirika la WWF limejikita katika kuhamasisha shughuli za utunzaji wa mazingira, rasilimali za maji, pamoja na maendeleo ya jamii, ikiwemo kilimo, ambapo limekuwa likishiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu na vifaa kwa wanajamii.

“Mto Ruaha Mkuu ndiyo chanzo kikuu cha maji katika bwawa la Mtera ambako kuna mitambo ya kuzalisha umeme na lengo kubwa ni kuhakikisha mto huo unatililisha maji kwa mwaka mzima” alisema ofisa maendeleo ya jamii msaidizi.

WWF huendesha Programu ya Maji (RWP) katika wilaya nane ambazo ni Iringa Vijijini, Kilolo, Mufindi, Njombe, Mbarali, Mbeya Vijijini, Chunya na Makete.

Hivi karibuni Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) kupitia Programu ya Maji Ruaha (RWP), mkoani Iringa lilikabidhi vifaa vya upaliliaji wa zao la mpunga kwa wakulima wa Kata ya Mlenge, Tarafa ya Pawaga wilayani Iringa.



Vifaa vilivyotolewa vitakavyosaidia kupalilia pamoja na kuwanufaisha wakulima wa mpunga wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mlenge, kutoka vijiji vya Kinyika, Isele, Kisanga na Magombwe.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...