Skip to main content

BREAKING NEWS....AJALI YA BASI NA LORI IRINGA YAUA ZAIDI YA WANNE LEO

 Basi  la kampuni ya Enuel lenye namba  za usajili T 919 DCD kulia  likiwa limegongana na lori usajili  T 122 ALW mali ya Trasisco ya  mkoani Arusha
WATU  wanne  wamefariki  dunia  papo  hapo na  wengine  zaidi  ya 20  kujeruhiwa  vibaya   baada ya  basi  la kampuni ya Enuel  Express kugongana  na  lori  eneo la   kijiji  cha Idetero wilaya ya  Mufindi mkoani  Iringa .

Ajali   hiyo  imetoka asubuhi  ya  leo  wakati basi hilo  likitokea Mbeya  kuelekea  Dodoma huku  mashuhuda  wa ajali  hiyo  wakidai  kuwa chanzo  cha ajali  hiyo ni uzembe  wa dereva wa basi  hilo ambae  alitaka  kuyapita magari mawili  yaliyokuwa  mbele  yake pasipo  kuchukua tahadhari .

Farida  John  ambae  ni  mmoja kati ya  abiria  waliokuwepo katika  basi hilo  alisema  kuwa  eneo  hilo ambalo ajali  imetokea  ni eneo ambalo  lina  mlima  mkali na  kuwa dereva  wa basi hilo  alikuwa akishuka na  Lori likipandisha  mlima  huo   na  kuwa  mbele  kulikuwa na basi na  lori  bovu  hivyo dereva wa basi hilo kuona   hivyo alizimika  kulitoa  basi hilo nje ya barabara  ndipo  walipogongana na lori  hilo.

Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Ramadhan  Mungi amethibitisha   kutokea kwa ajali  hiyo  mbaya na  kuwa  basi  hilo  lenye namba za usajili T 919 ACD  liligongana na  lori lenye namba za  usajili  T 122 ALW mali ya Trasisco ya  mkoani Arusha  likiwa na  tela namba  T 203 ATS ambalo  lilikuwa  likitokea Mafinga  kuelekea  Makambako mkoani Njombe.

Alisema  kuwa  mbele ya  basi  hilo  lililipata  ajali  kulikuwa na basi jingine  ambalo  liliongozana yote yakielekea  Iringa na baada ya  kufika  eneo hilo la ajali  kulikuwa na lori bovu lenye namba  T 647 ABK likiwa na tela lenye namba T 388 AYF  lililokuwa  limeharibika  eneo hilo  na  kupelekea   basi la mbele  kusimama  nyuma ya  lori   hilo  huku basi   hilo likijaribu  kutaka  kulipita lori  hilo .

" Wakati  dereva  wa  lori hilo akijaribu  kulipita  lori  hilo na basi ghafla  mbele  yake  aliona  lori  ambalo  lilikuwa  likija   mbele  yake   hivyo  katika  kuepusha kugongana  uso  kwa  uso ..... dereva  wa basi  aliamua  kulitoa basi  lake  nje ya barabara   upande  wa kulia na dereva wa  lori  ambalo  lilikuwa  likija  mbele yake nae  aliamua  kulitoa lori  hilo nje ya barabara  kushoto  na  ndipo  walipogongana nje ya  barabara  baada ya  wote  kukwepana  kugongana  uso kwa uso na kugongana nje ya  barabara "

Kamanda  Mungi  alisema  katika ajali  hiyo  abiria  wawili  waliokuwa katika  basi  hilo  walikufa  papo  hapo na  wengine ambao  idadi  yao bado  kufahamika   walijeruhiwa na  kukimbizwa katika  Hospital  ya  Mafinga  wilayani  Mufindi na baadhi yao  kukimbizwa Hospital ya  Makambako .

Hata   hivyo  alisema  kuwa katika  lori  hilo hadi majira ya saa 8 mchana    jitihada za  kuitoa  miili ya  watu  wawili  ambao  vichwa  vyao  vilikuwa  vikionekana  ilikuwa ikiendelea  japo  idadi kamili ya watu  waliokuwemo katika  lori  hilo bado haijafahamika  zaidi ya  watu  miili  hiyo miwili ambayo vichwa vilikuwa  vikionekana.

Hata   hivyo  alisema  taarifa  kamili na  idadi kamili ya  waliokufa na majina  yao  itatolewa mara  baada ya  zoezi la  kuitoa  miili ya  watu  hao  iliyobanwa katika lori  hilo kukamilika. (imehaririwa na Friday Simbaya)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...