Skip to main content

MWANDISHI WA HABARI ATANGAZA KUMVAA KAYOMBO MBUNGE WA MBINGA MASHARIKI

Humphrey Kisika

KWA vyovyote iwavyo, mapigo ya moyo ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mshariki mkoani Ruvuma, Gaudance Kayombo yataongezeka mara dufu baada ya kijana msomi; Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Humphrey Kisika (32) kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
 
Kisika, msomi mwenye shahada ya kwanza ya uandishi wa habari ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, anayesoma shahada ya pili ya uandishi wa habari na utawala anataka kuwania nafasi hiyo kupitia chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na wanahabari kijijini kwake Ukata, wilayani Mbinga, Kisika alisema anataka kupokea kijiti toka kwa mbunge huyo wa sasa ili atumie maarifa aliyonayo kusukuma zaidi maendeleo ya jimbo hilo.

Alisema anautambua na kuuthamini mchango wa mbunge wa sasa katika kusukuma maendeleo ya jimbo hilo lakini kuna haja akampokea kijiti hicho ili aongeze kasi yake.

“Kipaumbele changu kitakuwa maendeleo kwanza yatakayoshirikisha makundi yote ya jamii likiwemo kundi muhimu sana la vijana, yatakayonufaisha wote,” alisema.

Alisema endapo nia yake hiyo itatimia atahakikisha anaondoa pengo linalodumaza maendeleo baina ya wataalamu ambao ni watendaji wa shughuli mbalimbali za serikali na wanachi ambao ni wapiga kura.

“Kumekuwepo na manung’uniko toka kwa wananchi, lakini kimsingi manung’uniko hayo ynachangiwa sana na baadhi ya watendaji ambao kwa maslai yao binafsi au kwasababu ya kufanya kazi kwa mazoea wanashindwa kuutimikia vyema umma wa watanzania,” alisema.

Alisema CCM ina sera nzuri huenda kuliko chama kingine kile cha siasa ambazo hata hivyo yawezekana katika baadhi ya maeneo zimeshindwa kutekelezwa ipasavyo kwasababu ya uzembe wa wataalamu hao.

Akizungumzia muonekano wa kundi kubwa la vijana kuonekana wakishabikia zaidi vyama vya upinzani kuliko chama chake cha CCM, Kisika alisema katika mazingira ambayo nchi ina demokrasia ya hali ya juu kama Tanzania, ni lazima wawepo vijana wanaopenda vyama vya upinzani.

Hata hivyo alisema hiyo haina maana kwamba vijana wote wanavipenda vyama vya upinzani kwani CCM inao vijana wengi na ndio maana Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) upo imara kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa.

“Ombi langu kwa vijana wenzangu, ni muhimu katika kipindi hiki cha ushindani mkubwa wa kisiasa, tukafanya siasa kwa misingi ya upendo na amani, tusikubali kutumiwa kwenye harakati za siasa chafu zitakazohatarisha amani ya nchi hii ili Tanzania paendelee kuwa kisiwa cha amani,” alisema.


Endapo ndoto yake hiyo itatimia, Kisika alisema wana mbinga mashariki wategemee maendeleo ya pamoja yatakayoletwa kupitia nguvu ya pamoja.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...