Skip to main content

WANACHI WALALAMIKIA UGUMU WA MAISHA LICHA YA KUWA NA RASILIMALI ZA KUTOSHA



WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kasikazini akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI





Makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa, Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la mufindi kasikazini.





WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kasikazi akiwahutubia wananchi wa jimbo la mufindi kusini ambako anatarajia kugombea ubunge kupitia chadema.



Na Fredy Mgunda, Mufindi

Wananchi wa wilaya ya mufindi mkoani Iringa wamelalamikia ugumu wa maisha wanaokumbana nao kila kukicha licha ya wilaya hiyo kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali ya misitu pamoja na mazao ya biashara.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa wilayani mufind Williamu Mungai mmoja wa wananchi hao Clement Mwachang'a alisema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya inayofanya vema kwa kuingiza pato kubwa la taifa lakini wananchi wake wako katika wimbi kubwa la umaskini.



Mwachang'a amesema anashangaa wilaya kama ya mufindi inayoongoza kwa utoaji wa mbao nyingi lakini cha kushangaza shule nyingi za msingi hazina madawati jambo linalopelekea wanafunzi wengi kukaa chini.

"Hii ni aibu kubwa sana kwa wilaya yetu haiwezekani wilaya inarasilimali za kutoshalakini wananchi wake wengine wanashidwa hata kupata mlo mmoja kwa siku huku watoto wao wakishidwa kupelekwa shule kutokana na kushidwa kulipa ada ya kumuandikishia mtoto "


Kwa upande wake Williamu Mungai ambaye hivi karibuni ametangaza nia ya kulichukua jimbo hilo la mufindi kaskazi ambalo kwa sasa linaongozwa na naibu waziri wa maliasili na utalii Mahamudu Mgimwa amewataka wenyeviti wa mitaa kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shule za msinga hata kama hawana ada ya kuandikishiwa kwa kuwa elimu ni haki ya kila Mtanzania. 

Mungai alisema ni kila mtoto ana haki ya kupata elimu ya msingi kwa kuwa ndivyo katiba inavyosema na kuwataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarudisha majumba watoto kwa kisingizio cha kukosa hela ya kuwaandikishia.


"Niwatake wenyeviti wangu wa mitaa muhakikishe watoto wote wanaandikiswa na kama kuna mwalimu atagona kumuandikisha kwa kisingizio eti hana shilingi eflu hamsini jikusanyeni pamoja niiteni na mimi twende wote tuone kama hata muandikisha kwa maana walishasema elimu bure sasa bure waliyosema ikuwapi," alisema Mungai.


Hata hivyo mungai alisema imefika wakati wakuikomboa mufindi iliyoko katika wimbi la umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuataka wanamufindi kuhakikisha wanachagua viongozi wenye maono ya mbali katika kuwalete maendeleo na sio porojo za kila siku. 

Mungai alisema kuwa atahakikisha anazunguka vijiji vyote 72 vya wilaya ya mufindi katika harakati zake za kujenga chama na kuweza kutambua kero za wananchi na kuangalia ni jinsi gani ya kuzitatua .


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...