Skip to main content

TAMWA YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI JUU YA KUPAMBANA NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA


 WENCE AKITOA ELIMU KWA WANAHABARI WALIOKUTANA MKOANI IRINGA
 WANAHABARI NWAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MTOA ELIMU
 MWANAHABARI FRANK KIBIKI AKIWA MAKINI KUFUATILIA NINI KINACHOENDELEA KWENYE MAFUNZO HAYO

 NA fredy mgunda,iringa

Waandishi wa habari wametakiwa kuandika zaidi habari zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia hususan dhidi ya wanawake na watoto ili kuiamsha zaidi jamii inayowafanyiwa vitendo hivyo na mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya vitendo hivyo.


Msisitizo huo ulitolewa na chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kwa waandishi wa habari wa mikoa ya nyanda za juu kusini (IRINGA,MBEYA,SONGEA NA NJOMBE) ambapo wanahabari wameombwa kuendelea kufichua habari hizo hususan kwa wanaofanyiwa vitendo hivyo ili waweze kuelewa kwamba sheria dhidi ya ukatili huo zipo na kwamba kuna taasisi za kuwatetea.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mwanahabari wa siku nyingi WENCE MUSHI alisema dhahiri kuwa vitendo vya unanyanyasaji vimepungua kutokana na wanaofanya ukatili huo kuelewa, na watendewa pia kuzidi kuamka, juhudi zaidi zilitakiwa kujipenyeza zaidi dhidi ya imani za kimila ambazo bado zinashikiliwa katika sehemu mbalimbali za nchi.

“Endeleeni kutumia kalamu zenu na vifaa vyenu vyote kupiga vita vitendo vyote vinavyotokana na manyanyaso ya kijinsia ambayo hasa hutokana na mfumo dume,” alisema wence akiwaomba wahabari kufanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza juhudi za kutokomeza kabisa suala la unyanyasaji wa kijinsia.

Wence alisema jicho la waandishi wa habari linasaidia kuwaelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali yanafanywa kinyume cha seria,kuwaomba wanahabari kufanya habari za kichunguzi juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na unyanyasaji wake.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa kwa sasa TAMWA imekijita katika kufuatilia habari juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na mauwaji ya watu wenye ulemavu na kulenga hasa habari za kichunguzi ambazo zitaleta mabadiliko kwa jamii yetu.

Kwa upande wa waandishi wa habari wa nyanda za juu kusini walioshiriki warsha hiyo wamesema kuwa wanafanya kazi hiyo katika mazingira magumu,hivyo kuwaomba TAMWA kuwasaidia chombo cha usafiri kila mkoa ili waweze kuwafikia wananchi waliopo vijijini na kupata taarifa zao.

Lakini wakawataka wanahabri wengine kufanya kazi kwa kufuta weledi wao kutokana na elimu walioipata wakiwa darasa na kwenye mafunzo mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...