Skip to main content

MUUZA DUKA ATOKWEKA NA PESA ZA MWAJIRI WAKE...!


Edson Mwesigwa, 25 akiwa dukani siku ya mwisho.

MUUZA duka ya rejereja, Edson Mwesigwa miaka 25 mkazi wa Wilaya ya Misenyi  mkoani Bukoba amedaiwa kumwibia mwajiri wake fedha taslimu milioni 2.6 mauzo  ya MPesa usiku wa kuamkia tarehe 26/02/2015 na kisha kutokomea kusikojulikana.


Kijana huyo mwenyeji wa Kijiji cha Kigarama, Kata ya Kanyigo , Tarafa ya Kiziba wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera amedaiwa kumwibia mwajiri wake mauzo ya Mpesa nyumbani kwake Mtaa wa Wilolesi, Kata ya Gangilonga katika Manispaa ya Iringa mkoani Iringa.

Akiongea na Nipashe jana (IJUMAA) mwajiri huyo Edina Byemerwa  mkazi  wa Mtaa wa Wilolesi, Kata ya Gangilonga katika Manispaa ya Iringa alisema siku ya Ijumaa tarehe 26 mwezi Februari mwaka huu aliamka kama kawaida na kwenda kumgongea mtumishi huyo ili awahi kwenda dukani bila mafanikio.

Alisema kuwa alipoona kijana wake wa ndani hafungui mlango ndipo alipolazimisha kufungua mlango na kukuta chumbani kwake hakuwepo mtu na kwenda kumwambia mtoto wake ambaye wakati huo alikuwa anaoga bufuni na kusema  mbona kijana (Edson) hayupo.

Kijana wake ambaye ni mtoto wake ambaye alikuwa anaoga alisikika akisema akimwambia mama yake kuwa hapo sebuleni kuna begi lina hela ya mauzo ya Mpesa aliyeuza jana angalia kama lipo.

Lakini mama huyu alipoangalia vizuri sebuleni alikuta begi halionekani ndipo alirudi tena chumbani kwa mtumishi wa ndani kuchunguza na kukuta amebeba kila kitu kilichokuwa chake.

“Niliamka asubuhi na mapema na kwenda kumwamsha kijana wangu muuza duka la rejareja pale mjini na kukuta kijana chumbani kwake hakuwepo, ndipo nilirudi sebuleni tena kumuuliza mtoto wangu ambaye alikuwa anaoga bafuni kwamba mbona Edson hayupo chumbani kwake! Mtoto akaniambia niangalie begi hapo mezani lina mauzo ya  Mpesa ya jana kama lipo na kukuta kweli begi halipo…” alisema mwajiri huyo.

Hata hivyo, mwajiri huyo alisema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Iringa kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba IRI/RB/1678/2015 na polisi wameahidi kumpa ushirikiano.

Aliongeza kuwa kijana wa kazi (Edson )alitokea mkoani Bukoba nakuja kufanya kazi ya duka la rejareja mnamo tarehe 23/12/2014 na kwa sasa ni zaidi ya wiki tatu zimepita tangu mtumishi huyo atoweke nyumbani hapo.

“Kijana huyo alikuwa anauza vitu vya dukani na mtoto wangu wa kiume alikuwa anasaidia kuuza Mpesa hapo hapo dukani.

Alisema kuwa mtu yeyote atakayemuona atoe taarifa kituo cha polisi au kwa namba ya simu 0754917217 na kuongea kuwa donge nono litatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa kijana huyo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...