Skip to main content

RC: EPUKENI KUKIMBILIA UWEKEZAJI UPATU HARAMU...!




Mwenyekiti mtendaji wa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA), Charles Nchimbi (kushoto mwenye kapelo) akifuatilia ushiriki wa wawashiriki wa wanasemina wa kutoka chama cha viziwi mkoani Iringa wakati meneja uhusiano kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji (CMSA) Charles Shirima (hayupo picha) akitoa mada ya dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji kwa chama cha viziwi tanzania jana. (Picha na Friday Simbaya)



Washiriki kutoka chama cha viziwi mkoani Iringa wakifuatilia semina ya mafunzo kwa umakini kuhusu dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji jana iliyoandaliwa na mamlaka ya mitaji na dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na taasisi ya maenedeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA) hapa mkoani Iringa. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima akitoa mada wakati wa semina ya mafunzo kwa chama cha viziwi Tanzania kuhusu dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji jana iliyoandaliwa na mamlaka ya mitaji na dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na taasisi ya maenedeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA) hapa mkoani Iringa. Kulia ni mkalimani lugha ya alama. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


Meneja Uendelezaji wa Masoko ya Mitaji (CMSA), Nicodemus Mkama akitoa mada wakati wa semina ya mafunzo kwa chama cha viziwi Tanzania kuhusu dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji jana iliyoandaliwa na mamlaka ya mitaji na dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na taasisi ya maenedeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA) hapa mkoani Iringa. Kulia ni mkalimani lugha ya alama. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)


MKUU wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amewaasa wananchi kuepuka kukimbilia uwekezaji wa kutengeneza hela nyingi kwa haraka.

Alisema hali hiyo huwa inasababisha watu wengi kutapeliwa fedha zao na kujiingiza kwenye biashara na uwekezaji usio halali na mara nyingine kujikuta wanavunja sheria na kujiunga na michezo ya upatu haramu na kupoteza fedha zao.


Masenza alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua semina kwa wanachama wa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania (TAMAVITA) kuhusu ushiriki na uwekezaji katika masoko ya mitaji Tanzania (CMSA).

Semina hiyo iliandaliwa na mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA). Alisema kuwa michezo ya upatu haramu ni kinyume cha sheria na imeharamishwa.

Mkuu huyo wa mkoa waliwaasa wanasemina kutumia vyema elimu walioipata kama mwanga wakuelewa ni vitega uchumi vipi vinavyopatikana katika sekta ya masoko ya mitaji.

Hivyo kuainisha njia ya uwekezaji sahihi na zile sizizo sahihi kama vile upatu haramu, mfano dollar jet, DECI, na mengine iliyowahi kutokea hapa nchini.

Alisema kuwa azma ya serikali kujitoa katika umiliki na uendeshaji wa njia kuu za uchumi na kutoa fursa kwa wananchi wake kumiliki kampuni ambazo awali zilikuwa chini ya uongozi wa serikali.

“Kati ya hatua zilizochukuliwa na serikali ni kuanzishwa kwa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana kama msimamizi mkuu wa mfumo wa masoko ya mitaji,” alisema Masenza.

 Alisema kuwa serikali kwa kupitia vyombo vyake kama CMSA iko makini katika kuangalia na kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kushiriki katika mfumo wa masoko ya mitaji na pia mslahi yake yanalindwa kwa kuzingia taratibu za kisheria na kibiashara bila kwuwepo kwa upendeleo.

Aidha, mkuu wa mkoa huyu aliupongeza uongozi wa mamlaka ya mitaji na dhamana kwa kuandaa na kuendesha semina muhimu hasa ukizingatia kuwa sio wananchama wa chama cha viziwi pekee walio na shauku ya kujifunza, bali hata wafanyabiashara, wafanyakazi, wanataaluma na wananchi wengi bado dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji ni ngeni kwao.

Kwa upande wake, meneja uendelezaji wa masoko ya mitaji Tanzania, Nicodememus Mkama alisema lengo na dhumuni ya semina hiyo ni kutoa elimu kwa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania ili wawe mabalozi watakaotumika kutoa elimu kwa wanachama wao.

Alisema kuwa chama cha viziwi Tanzania kina wanachama zaidi ya milioni moja na kina matawi nchi nzima, kwa hivyo wanasemina waliyopata elimu hiyo watatumika kama mabalozi kutoa elimu ya dhana ya uwekezaji katika masoko ya mitaji kwa wenzao.

Pia, alisema kuwa  masoko ya mitaji yanawawezesha wawekezaji kufaidika kwa njia nyingi kama vile kuweka akiba kwa kuiwekeza na kuongeza kuwa kununua hisa ni kuwekeza matumizi ya baadaye.

Faida nyingine ni kuwezesha umiliki wa makampuni kwa umma pamoja na hisa zinazoweza kuwekwa rehani kupata mkopo.

Alisema hii ni faida nyingine nzuri kwa wanahisa kutumia hati ya umiliki wa hisa kama rehani na kupata mikopo katika taasisi za kifedha.

Hata hivo, Mkama alisema kuwa hii ni semina ya pili kwa chama cha viziwi Tanzania baada ya semina dhana ya uwekezaji katika mipango ya uwekezaji wa pamoja kwa wanachama wa taasisi ya maendeleo ya viziwi iliyofanyika kule Songea mkoani Ruvuma mwezi huu.

Alisema kuwa licha ya changamoto zinazowakabili za ulemavu wa kusikia kundi hili lina mwamko wa kukamata fursa za uwekezaji katika masoko ya mitaji na kuchangia ukuaji wa pato la kila mmoja na uchumi wa taifa kwa ujmla.

Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) ilianzishwa mwaka 1995 kwa sheria ya bunge namba 5 ya masoko ya mitaji na dhamana ya mwaka 1994.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...