Skip to main content

TAHARIRI: JUHUDI HIZI ZA WAZIRI MKUU PINDA KUSAIDIA SHULE ALIYOSOMEA ZIUNGWE MKONO




Picha juu na chini ni baadhi ya majengo yaliyokamilika ya Shule ya msingi Kakuni yaliyojengwa na Waziri Mkuu Pinda kupitia michango ya wadau wa maendeleo.

Na Andrew Chale 

Kila mmoja wetu anatambua mchango mkubwa wa elimu hasa ile inayotolewa ikiwemo ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari na elimu ya juu ikiwemo chuo. Pia katika hilo ni jamb la msingi sana na la maana hasa unapokumbuka mahala ulipopatia elimu husika.

Mtandao huu tunapenda kuungana na kumpongeza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa juhudi zake za dhati kabisa katika kuhakikisha shule yake aliyowahi kusoma hapo inasaidiwa na kufikia malengo yake.

Waziri Mkuu alipaata elimu yake katika Shule ya msingi Kakuni. Kwa kusoma hapo darasa la kwanza hadi la nne. Lakini kwa mapenzi mema na juhudi za kutaka kuona watoto wa hali ya chini hasa wa wakulima wanapata elimu bora, kwa juhudi zake binafsi, ameweza kusaidia shule hiyo ikiwemo kutafuta wafadhili mbalimbali wa kuipiga tafu, akiwa kama Mizengo Pinda. Ambapo unaweza kusoma kiunganishi hichi hapa cha mtandao ili kusoma habari hiyo zaidi ya wadau kumuunga Waziri Mkuu Pinda katika kuisaidia shule ya Kakuni:


Mtandao huu unapongeza juhudi hizo za Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivyo pia nawe ukiwa ni miongoni mwa unayeguswa na maendeleo ya elimu hapa nchini, ni wakati wa kutembelea shule yako uliosoma awali iwe elimu ya ‘vidudu’ yaani Chekechea/Awali, Shule ya Msingi ama Sekondari basi ni wakati wa kurejea na kusaidia chochote kile ili kuendeleza Elimu hapa Nchini.

Bila shaka kama Watanzania tutaiga juhudi hizi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda, bila shaka elimu ya Tanzania itapanda maradufu kwani tumeweza kushuhudia kwa upande wa juhudi hizo za Mizengo Pinda ikiwemo kushawishi wadau ikiwemo Serikali ya Japan, kutoa msaada wa dola za Marekani, 90,286, ambazo ni sawa na Sh. Milioni 160.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Awali kwenye Shule ya Msingi, Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda.

Juhudi za Mizengo Pinda za kuanzisha wazo hilo la kusaidia kuijenga shule yake ni kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. 

Kwani alipata kusoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.

Hivyo, tunatambua wapo wasomi wengi, wapo wabunge, wapo Mawaziri, wapo Wakurugenzi na wengine wenye vyeo vikubwa Serikali, sekta binafsi na waliopo ndani nje ya nchi, shime tujitokeze kwa wingi kwa kila mmoja kwenda kwenye shule aliyosoma na kuchangia chochote.

Tunatambua sisi tumepata elimu wakati gani na kiwango cha elimu wakati huo kilikuwaje, hivyo tutakapojitokeza kama alivyofanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hii itasaidia kukuza elimu yetu hapa Nchini.


Muonekano wa majengo yaliyokamili ya shule ya msingi Kakuni alipopata elimu ya msingi Waziri Mkuu Pinda na kuamua kuijenga upya kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.3/- kutokana na michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...