Skip to main content

MEYA JERRY SLAA AIZAWADIA PIKIPIKI TIMU GONGO LA MBOTO

Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki lililoandaliwa na Lucas Lutanilwa.

Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki timu ya Mazombi FC lililoandaliwa na Lucas Lutanilwa.
Mwakilishi wa Timu ya Vijana Jogging Club akipokea zawadi ya fedha baada ya kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto.
Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akizungumza kabla ya kuanza kwa mtanange huo kati ya Timu ya Mazombi FC na Sobibo FC.

Washindi wa nne wakipokea haki yao pia.
Washindi wa nne wakipokea haki yao pia.
Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akifuatilia mpambano kati ya Timu za Mazombi FC na Sobibo FC. Mazombi walifanikiwa kutaa ubingwa baada ya kuifunga Sobibo 1-0.

Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa () akikagua timu ya Mazombi FC kabla ya mpambano kuanza.


Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akikagua timu ya Sobibo FC kabla ya mpambano kuanza.

Timu ya Sobibo FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.

Timu ya Mazombi FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.
Mashabiki mbalimbali wa Gongo la Mboto wakifuatilia mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto.

Baadhi ya wachezaji na mashabiki na Timu ya Vijana Jogging Club wakishangilia baada ya kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto.

Na Mwandishi Wetu

MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa jana alilazimika kutoa zawadi ya pikipiki baada kuvutiwa na ushindani mkubwa uliokuwepo katika mchezo wa fainali wa mpira wa miguu kugombea pikipiki aina ya Boxer.

Meya Slaa alilazimika kutoa pikipiki hiyo baada ya timu za Mazombi FC na Sobibo FC zote za Gongo la Mboto kuonesha ushindani mkali katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Kampala Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Slaa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ameahidi kuwakabidhi pikipiki mpya timu ya Sobibo FC ambayo ilishika nafasi ya pili katika mchezo huo wa fainali ambapo timu ya Mazombi FC iliibuka mshindi na kukabidhiwa pikipiki mpya aina ya Boxer iliyotolewa na muandaaji wa mashindano hayo Lucas Lutanilwa.

"...Kutokana na ushindani mkubwa uliooneshwa na timu zote mbili natamka kwamba hata washindi wa pili Sobibo FC nao ninawazawadia pikipiki kama waliopata wenzao ili kuleta kiu ya kupenda michezo zaidi kwa vijana wetu," alisema Slaa akizungumza alipokuwa akikabidhi pikipiki kwa mabingwa Masombi FC.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa pande zote mbili timu ya Mazombi imefanikiwa kutwaa ubingwa na kukabidhiwa pikipiki mpya baada ya kuifunga Sobibo FC goli 1-0 lilipatikana dakika 70 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.

Timu zote mbili pia zilikabidhiwa seti mojamoja ya jezi kwa kuweza kufika fainali, hata hivyo washindi wa nne na tatu wa Mashindano hayo yaliyopewa jina la Luta Cup walipewa zawadi za fedha taslimu kama pongezi. Timu ya Vijana Jogging Club walifanikiwa kutwaa ushindi wa tatu na kujinyakulia fedha taslimu katika mashindano hayo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...