Skip to main content

MKOA wa Iringa kuandikisha jumla ya wapigakura 646,575 katika daftari la kudumu ya wapigakura

semina ya mafunzo ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura iliyohusisha mratibu wa uandishaji wa mkoa, afisa mwandishaji, maafisa waandishaji wasaidizi na maafisa uchaguzi wa halmashauri kwa Mkoa wa Iringa.

MKOA wa Iringa unatarajia kuandikisha jumla ya wapigakura 646,575 katika daftari la kudumu ya wapigakura kwa kutumia mfumo mpya ujulikanao kama Biometric Voters Registration (BVR) unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu, Nipashe imedhibitisha.


Hayo wamefahamika jana wakati wa semina ya mafunzo ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura iliyohusisha mratibu wa uandishaji wa mkoa, afisa mwandishaji, maafisa waandishaji wasaidizi na maafisa uchaguzi wa halmashauri kwa Mkoa wa Iringa.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo/jana Katibu Tawala Msaidizi-Serikali za mitaa ambaye pia mratibu wa uchaguzi wa mkoa wa Iringa, Wilfred Myuyu alisema kuwa katika maoteo (projection) ya awali mkoa unatarajia kuandikisha wapigakura wapatao 646,575 pamoja na vituo vya uandishaji 1,192.

Alikitoa mchanganuo wa uandikishaji kwa kila halmashauri alisema kuwa Manispaa ya Iringa inatarajia kuandikisha wapigakura 79,086, Halmashauri ya Iringa (121,452), Halmashauri ya Mufindi (252,303), Mafinga mjini (74,043) na Kilolo (118,692).

Kwa upande wa vituo vya uandikishaji katika mabano Manispaa ya Iringa itakuwa na vituo (192), Kilolo (257), Mufindi DC (347), Mafinga TC (76) na Iringa DC (320).

Awali wakati akifungua semina ya mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Angelina Mabula kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alitoa wito kwa maafisa hao kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na tume ili kuweza kufanya kazi vizuri wakati wa zoezi hilo.

“Napenda kusisitiza tena kwenu kwamba mkiwa maafisa waandishaji na maafisa wasaidizi mnatakiwa kuhakikisha kwamba watu wote wanaostahili kuandikishwa na watakaofika kujiandisha kwenye vituo wanandikishwa na kuhudumiwa kulingana na utaratibu uliowekwa ili majina yao yawepo katika daftari la kudumu la wapigakura,” alisema Masenza.

Aidha, katika utaratibu wa sasa, kama ilivyokuwa katika utaratibu wa zamani, wawakilishi wa vyama vya siasa wanataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapigakura.

“Jambo hili ni muhimu kwani linasaidia kudhihihirisha uwazi katika zoezi zima. Wajibu wa wawakilishi wa vyama vya siasa kama ilivyoelezwa ni kuangalia kwamba sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa na tume (NEC) zinazingatiwa katika uandikishaji,” alisema mkuu huyo.

Hata hivyo, mkuu wa mkoa huyo alitoa wito kwa viongozi wa dini kuhamasisha waumini na watu wote hususan raia wote walio na sifa za kujiandikisha kupiga kura ili wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuandikishwa.

Aliongeza kuwa watakaojiandikishwa ni wananchi wote waliowahi kuandikisha hapo awali, waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na wote ambao kwa sababu mbalimbali hawakuwahi kuandikishwa ikiwa ni pamoja na wale watakaotimiza umri wa miaka 18 ifikapo siku ya uchaguzi, yaani Oktoba 2015.

BVR ni kifaa cha kisasa ambacho huandikisha kwa kutumia kompyuta na kuchukua alama za vidole, saini na upigaji picha kwa ubora wa hali ya juu ili kuondoa uwezekano wa wapiga kura kujiandikisha zaidi ya mara moja.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...