Skip to main content

LUKUVI APATA MPINZANI JIMBO LA ISIMANI

WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI




WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI


NA RAYMONDI MINJA, IRINGA


MSOMI wa Digri ya uhandisi wa kilomo na mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA) Mhandisi Sebastiani Kayoyo (39) anetangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika jimbo la Isimani kwa tiketi ya CCM linaloshikiliwa na Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi.

Akitangaza nia yake hiyo mkoani Iringa juzi Kayoyo alisema kujitosa katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.

Kayoyo alisema kuwa siko kwamba mbunge aliyeko madarakani hajafanya mambo ya msingi ila mbunge huyo ameongoza jimbo hilo kwa miaka mingi hivyo ni fursa ya hazina kubwa ya vijana walioko ndani ya chama cha mapinduzi kuweza kushika hatamu katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika nchii hiii.

"Mbunge anayeshikiria jimbo ninamheshimu sana na ameweza kufanya mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia nina kuwa na Haki ya msingi kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi waliokosa fursa mbalimbali" kayoyo Kakoyo ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kama muhandisi wa kilimo (Mtaalamu wa zana za kilimoba kilimo cha umwagiliaji )ni mzaliwa wa kijiji cha Tungamalenda kata ya idodi tarafa uya idodi iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani Alipoulizwa kuhusiana na hatima ya ajira yake endapo ataukosa ubunge,”Mimi ni mtumishi wa serikalini ninajua taratibu zote za utumishi serikali lakini niko tayari kuacha kazi ili kufanyakazi na ndugu zangu wa Isimani katika kujiletea maendeleo”

Akitaja vipaumbele vyake endapo chama chake kitampa ridha ya kukimbiza kijiti hicho Kayoyo alisema kuwa ataweka msisitizo katika swala la afya , kilimo ,maji safi na salama pamoja na swala la miundombinu ikiwemo Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa kwa kuwa jimbo hilo halijawahi kuwa na lami tangu nchii hii ilipopata uhuru wake

"Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, napenda kuona wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza wajibu" alisema Kayoyo.

Kwa kujitokeza huko kwa Kayoyo kunafanya idadi ya wagombea kutoka chama cha mapinduzi CCM kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo,

Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza huku kwa upande wa chadema mbunge wa viti maamulu Chiku Abwawo pamoja makamu mwenyekiti wa bavicha Ole Sosopi.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...