Skip to main content

Nyota ya Kibiki yazidi kung’ara Ubunge Iringa mjini



NA MWANDISHI WETU

MATOKEO ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Southern Zone Election Research (SZER), katika jimbo la Iringa mjini umeonyesha kuwa nyota ya Mwanahabari , Frank Kibiki pichani aliyetangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) inazidi kung’ara baada ya kuongoza huku akichuana vikali na Mbunge wa sasa Mchungaji Peter Msigwa(CDM).

Utafiti huo uliofanywa kwa miezi minne tangu, kuwepo kwa wimbi la watu wengi kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa mjini, wakiwemo makada lukuki wa CCM unaonyesha kuwa Nyota ya Frank Kibiki inazidi kung’ara kutokana na kuungwa mkono na makundi mengi ya kijamii hasa vijana, wanawake, walemavu na wazee.

Akizungumza na mtandao huu, Mtafiti mkuu wa SZER, Patson William alisema utafiti huo umefanywa katika kata 14 za jimbo la Iringa mjini huku wagombea vijana wakiwa ndio wanaoongoza kupendwa ikilinganishwa na wagombea wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.

Kibiki anaongoza kwa asilimia 40.7, Mchungaji Msigwa 20.9, Jesca Msambatavangu 11.7, Dr Yahaya Msigwa 7.6, Fredrick Mwakalebela 2.8, John Kiteve 2.4, Mahamoud Madenge 1.2 na wengine waliobaki wanagawana asilimia 12.7.

Utafiti huo unaonyesha kuwa, kinachomfanya Kibiki kuendelea kung’ara ni siasa zake za kistaarabu, taaluma ya uana habari, uwezo mkubwa wa kujenga na kujibu hoja anazokumbana nazo sambamba na uzoefu katika utendaji wake wakati akiwa Katibu wa UVCCM katika wilaya mbalimbali alizowahi kufanya kazi.

Alisema utafiti huo umefanywa kwa njia ya madodoso ambapo watu 400 walijibu na maswali ya papo kwa papo ambapo watu 1000 waliyajibu.

Alitaja kata zilizohusishwa kuwa ni Makorongoni, Miyomboni/kitanzini, Kihesa, Kwakilosa, Mlandege, Mivingeni, Gangilonga, Kitwiru, Igumbilo, Nduli, Ruaha, Mkwawa, Mtwivila na Isakalilo.

Mambo ya msingi ambayo utafiti huo uliangalia ili kutafuta majibu ni Changamoto za jimbo la Iringa mjini kwa sasa,sifa za Mbunge anayetakiwa kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la atakayesimamia vizuri changamoto hizo na mazingira ya siasa za sasa za jimbo la Iringa mjini.

Hata hivyo CCM na Chadema ndiyo vyama pekee vinavyochuana kwa kasi katika jimbo la Iringa mjini, tangu CDM iliponyakua jimbo hilo mwaka 2010.

Hata hivyo utafiti huo unaonyesha kuwa CCM itakuwa na wakati mgumu ikiwa watateua jina la mtu asiyechaguo la wananchi jambo ambalo, litampa Mchungaji Msigwa ushindi usio na jasho.

“Utafiti huu unaonyesha kuwa CCM inanafasi nzuri ya kuchukua jimbo la Iringa mjini ikiwa tu watafuata nini wana Iringa wanasema vinginevyo, nafasi ya Msigwa kuendelea itakuwa kubwa,”anasema

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...