Skip to main content

Stendi kuu mjini Iringa waanzisha timu ya mpira wa miguu ya KIBIKI FC


Kibiki azizungumza na kijana, fundi viatu wa mjini Iringa!




Na mwandishi wetu, Iringa



VIJANA wa stendi kuu ya mabasi ya mjini Iringa, wameanzisha timu ya mpira wa miguu ya ‘Kibiki Football Club’ili kuunga mkono harakati za mwanahabari wa gazeti la Uhuru na mzalendo, baada ya kutangaza nia kuwania jimbo hilo.

Katibu wa timu hiyo, Charles Manet alisema wameamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu inayoitwa Kibiki, ili kuonyesha dhamira yao ya dhati katika kumsaidia kijana mwenzao.

“Yeye mwenyewe hakujua kama tumetumia jina lake kwenye timu yetu, tayari tumeshacheza mechi mbili tangu timu yetu ianze kuitwa Kibiki FC na tunatarajia kuendelea kucheza mechi za kirafiki, tukianza na timu ya Wambi ya stendi kuu ya mjini Mafinga,”alisema

Maneti alisema wamekuwa wakisafiri kwa kuchangishana fedha na kwamba tayari wamepata jezi seti moja, kutoka kwa wadau mbali mbali wa michezo mjini Iringa.

Aliwataka wapenzi wa soka la mjini Iringa kuunga mkono jitihada za vijana hao katika kuhakikisha, timu hiyo inasonga mbele badala ya kuikatisha tama.

“Pamoja na kukatishwa tama tangu tuunde timu hii lakini ukweli ni kwamba, hatutaacha kwa sababu Kibiki ni kiongozi na tusipomuunga mkono kijana mwenzetu tutakuwa hatujamtendea haki hata kidogo,”alifafanua.

Kabla ya kuunda timu hiyo vijana hao, walichangishana fedha zaidi y ash laki moja na kumkabidhi Kibiki, wakimtaka azitunze kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Iringa, muda ukifika.

Wakizungumzia ubunge, vijana hao walisema kuwa jamii ya wana Iringa inatarajia kumpata kiongozi anayetokana na wenyewe, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wampigie kura ya kuwa mbunge wa jimbo hilo na sio vinginevyo.

Tangu alipotangaza nia ya kuwania jimbo hilo, Kibiki amekuwa akikubaliwa na makundi mbalimbali wakiwemo vijana, walemavu, wanawake na wazee.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...