Skip to main content

TAKWIMU ZAKWAMISHA UPATIKANAJI WA MAENDELEO



Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Bi Amina Shabani akifungua semina ya siku moja ya kujadili mpango utekelezaji wa Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG’s, iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar na kuwashirikisha Maofisa Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi wa Taasisi zisizo za Kiserekali, ulioandaliwa na Tume ya Mipango Zanzibar na Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania na kufadhiliwa na UNDP.




Na Mwandishi wetu, Zanzibar

UKOSEFU wa takwimu sahihi katika masuala mbalimbali umeelezwa kuchangia kutopiga hatua kwenye mipango ya kimaendeleo inayopangwa na serikali juu ya wananchi.

Aidha upotoshaji wa takwimu hizo unaofanywa na baadhi ya watendaji kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe pia umekuwa ukichangia kuchelewa hatua za kimaendeleo.

Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, Amina Shaaban wakati akifungua semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mjini hapa.

Amina alisema, kuwa takwimu ndiyo zinaonesha hali halisi na pia zinawezesha fedha kutoka kulingana na mahitaji, hivyo ni muhimu kuzingatiwa kwa jambo hilo ili mipango ya maendelo iweze kufanyika kwa wakati.

"Kulikuwa na kamati ile ya ufundi na ya muda, siku hizi hazipo kama zimekufa ni vyema zikarudishwe tena maana zilikuwa na jukumu la ufuatiliaji na kutukumbusha mara kwa mara," alisema Amina.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk. Oswald Mashindano alisema, semina hiyo inalenga kujadaili utekelezaji wa malengo ya millenia kabla ya kumalizika Septemba, mwaka huu na ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu.

Aidha alisema, nchi nyingi hazijakuwa na uwezo wa kutekeleza malengo ya millenia ikiwemo Tanzania, hivyo kutokana na hali hiyo ilikubalika kuwepo kwa ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu.

"Kwa sisi Tanzania kidogo tuna bahati ya kuiga hatua kidogo, lakini pamoja na kutimiza baadhi ya malengo, bado kuna maeneo ambayo hatujafanikiwa sana na moja kati ya sababu iliyofanya tukwame ni pamoja na ukuaji wetu wa uchumi," alisema.

Akizungumzia kuhusu kamati za ufundi na ya muda, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiamatifa wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy alisema, kuwa suala hilo atalirudisha kwenye tume ya mipango ya Tanzania Bara ili liweze kushughulikiwa kwa wakati.

Hata hivyo alisema, ili nchi iweze kupiga hatua katika mikakati ya maendeleo ni muhimu kwa sekta binafsi kushiriki kwa mstari wa mbele kutokana na kuwa nafasi kubwa katika kuendeleza maendeleo na uchumi wa taifa.

"Sekta binafsi wao ndiyo wenye pesa nyingi sana kuliko serikali, ukiangalia hata katika nchi zilizoendelea sekta binafsi kwa kiasi kikubwa zimechangia sehemu kubwa ya maendeleo yao," alisema Balozi Mushy.

Balozi Mushy alisisitiza umuhimu wa takwimu sahihi kwa kuwa ndiyo silaha pekee katika kufanikisha mipango ya kimaendeleo kukamilika kwa wakati.

Semina hiyo iliwashirikisha wataalamu wa tume ya mipango ya Zanzibar na tasisi zingine za serikali ilikuwa inalenga kuwajengea uwezo na kujadili ajenda 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na mipango ya maendeleo baada ya kukamilika kwa Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs) Septemba, mwaka huu.









Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hutuba ya Katibu Mtendaji Bi Amina Shabani akifungua mkutano huo.









Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Anna Senga akitoa salamu za Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG's.









Washiriki wakiwa katika ukumbi wa Mkutano hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. wakifuatilia mada zinazotolewa wakati wa mkutano huo.









Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG's Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.









Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia kwa utulivu michango na mada zilizoku zikiwasilishwa.









Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.








Balozi Celestine Mushy akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo .









Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akiwasilisha mada ya "Elucidating SDG 17 on means of implementation and Global Partnership for Development and Financing of Post MDG's Development Agenda".





Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia mada zinazowasilishwa na wahusika.







Dk. Kenneth Mdadila, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Idara ya Uchumi akiwasilisha mada ya "Tanzania's preparedness in Monitoring Sustainable Development Goals- Analysis Based on Global Indicator Framework" katika semina hiyo..



Pichani juu na chini ni washiriki wa semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar.






Pichani juu na chini ni Maofisa mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakishiriki kuchangia mada katika semina hiyo ya siku moja iliyofadhiliwa na UNDP.







Mdau Yasser Manu kutoka ESRF.








Washiriki wakichangia mada zilizowakilishwa wakati wa semina ya siku moja iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...