Skip to main content

UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI





Head of India Tanzania Center of Excellence in ICT (DIT), Dr. Amos Nungu akiwakaribisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika kwenye mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao.(Picha zote na Geofrey Adroph wa pamoja blog).




Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa anayeshughulikia na masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (wa kwanza kutoka kushoto) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao kwa walimu wa vyuo vya elimu




Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari akifungua mafunzo kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO yaliyofanyika jijini Dar.




Bi. Eunice Gachoka kutoka Kenya Institute of Curriculum Development akijitambulisha kwa walimu (hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya kupitia mtandao.




Daudi Mbona mkufunzi kutoka chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu walioudhuria mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika kwenye chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini Dar.





Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.








Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo.



Na Geofrey Adroph, Pamoja blog

UNESCO imeaandaa mafunzo ya uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama.

Hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini Tanzania hivyo kuona kama kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama hasa katika vyuo hivyo.


Baada ya kuona kuna mapungufu hayo UNESCO waliamua kuanzisha mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wakishirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania waliamua kuanzisha mradi huo kwa malengo makuu matatu ambayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia na kujifunzia, Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo alivitaja vifaa hivyo kwa kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta, Projecta, na Sola ili kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika ufundishaji wa masomo hayo .

Kupitia mradi huo wa (CFIT), UNESCO imeandaa mafunzo ya siku tano kwa walimu wa vyuo vya ualimu kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu hapa nchini Tanzania ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika ukuzaji wa Tehama hasa kupitia kwenye njia ya mtandao na pia kuendana na wakati kutokana na mabadiliko pamoja na ukuaji wa matumizi ya Teknolojia

Mafunzo haya yaliyoandaliwa na UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya walimu wa vyuo ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama.

Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Daudi Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT) na Godfrey Haongo kutoka Open University of Tanzania ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa .

Waalimu tisa kutoka chuo cha ualimuTabora, waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District, pia kuna baadhi ya watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara ya elimu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.

Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kitehama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...