Skip to main content

UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI

Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya matumizi ya Tehama katika ufundishaji kwenye vyuo vya ualimu.



Na Geofrey Adroph, Pamoja blog

Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu ya Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limejikita katika uboreshaji wa elimu kwa kuwapa mafunzo walimu katika somo la Teknnolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Akizungumza leo katika Ufungaji wa Mafunzo yaliyoandaliwa na UNESCO wakishirikiana na China Funds in Trust Project (CFIT) yaliyofanyika kwa siku tano katika Ukumbi wa DIT, Jijini Dar es Salaam, Ofisa Miradi wa UNESCO, Faith Shayo amesema mafunzo waliopata walimu wa vyuo vya walimu mbalimbali nchini itawasaidia katika uboresha wa elimu ikiwa ni pamoja na kuwapa vifaa vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo.

Faith amesema ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini kuona kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama katika vyuo vilivyopo nchini.

Amesema katika kufikia malengo ya mradi wa UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wanaoshirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini kwa malengo makuu matatu.

Aliyataja malengo hayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika somo la Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia.

Faith amesema baada ya mafunzo hayo vyuo vitapata vifaa mbalimbali ambayo ni kompyuta, Projecta,ya na vifaa vya kuzalisha umeme wa jua (Solar Energy) kwa ajili ya kuondokana na tatizo umeme unaokatika katika mara kwa mara.

Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT), Daudi Mboma pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Godfrey Haongo ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa .

Waliopata mafunzo hayo Waalimu tisa wa Chuo cha Ualimu Tabora, na tisa wengine kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, na mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District.

Mafunzo hayo yametolewa kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya elimu ambao wana mchango mkubwa hasa katika ukuzaji wa Tehama wakishirikiana na wanafanya kazi wa UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini. 

Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kitehama katika taifa kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...