Skip to main content

WAKUNGA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KUTENGENEZA TAIFA LA KESHO




Rais wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga akimkaribisha Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges (kulia) kuzungumza na wakunga nchini waliokusanyika kwenye mdahalo wa siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Musoma mkoani Mara. Kushoto ni Kaimu Muuguzi mkuu wa serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi wetu, Musoma

Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges, ametoa wito wa wakunga na wauguzi kubadilisha uzoefu wa shughuli zao ili kuhakikisha taifa linaondokana na vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Akizungumza katika mdahalo kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya wakunga duniani, iliyofanyika kitaifa mkoani Mara, Ganges alisema kwamba ni wajibu wa wakunga kuhakikisha kwamba dunia ya kesho inakuwa bora na wanaweza kwa kushirikiana na kubadilishana uzoefu.

Alisema dunia inawategemea wauguzi kuendeleza kizazi cha binadamu na katika kufanya hivyo kuna changamoto nyingi zinazotokea changamoto ambazo zinaweza kumalizwa kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika eneo analofanyia kazi.

Aliutaja wajibu huo kama uongozi, uelimishaji na pia utendaji wa kazi wenye tija na busara.

Alisema nia ya siku ya wakunga ipo wazi ni kuleta ushirikiano kwa ajili ya kuleta dunia iliyo njema ya kesho.

Mtendaji huyo wa Shirikisho hilo lenye makao makuu yake nchini Uholanzi alisema kwamba wanafuraha kubwa kusikia mambo makubwa yanayofanywa na wakunga nchini Tanzania pamoja na changamoto zake zilizopo.

Alisema mafanikio yaliyopo ni matokeo ya ushirikiano na ufanyaji kazi wa pamoja.


Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges akizungumza na Wakunga nchini Tanzania waliohudhuria kwenye mdahalo wa siku moja uliofanyika kwenye ukumbi wa Mara ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mara mjini Musoma kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga duniani kujadili changamoto zinazowakabili Wakunga nchini. Katikati ni Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy Mwanga na Kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikalim kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala.

Alisema katika hotuba yake hiyo kwamba wakunga wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wanazaliwa salama, wanawake wanakuwa salama na kizazi cha binadamu kinakuwa salama.

Wakati huo huo Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) Felista Bwana amesema tafiti zilizopo zinaonesha kuwepo na idadi ndogo ya wakunga wataalamu na kwamba juhudi lazima zifanyike kuhakikisha kwamba vituo vya afya vyote vina wakunga wataalamu.

Aidha mratibu wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy alisema chama hicho chenye wanachama 3000 miongoni mwa wakunga wauguzi elfu 39 kimelenga kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa anapata huduma za mkunga mtaalamu .

Alisema kwa sasa ni asilimia 51 tu ya wanawake wazazi wanapata huduma ya wakunga wataalamu.

Alisema ipo haja ya kukubaliana kuwekeza kwa wakunga kwa ajili ya taifa la kesho.

Naye Daktari bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Rosina Lipyoga akizungumza katika siku hiyo ya wakunga alisema ni aibu kwa watoto na wazazi kufa kutokana na huduma hafifu.

Aliwataka wakunga kutumia maarifa zaidi kuokoa maisha ya watoto na wazazi kwa kuwa na maamuzi ya haraka yanayozingatia uwezo wa eneo analofanyia kazi na kuhakikisha, kazi zisizowezekana zinapelekwa katika hatua afiki.

Alisema ipo haja ya mara kwa mara kwa wakunga kuangalia mabadiliko mbalimbali ya kazi zao kwa kufuatilia wenzao wamefanya nini na sasa tatizo analoshughulikia wengine wamelifanyaje.

Alisisitiza haja ya ufanyaji maamuzi mapema ili kuokoa maisha ya mtoto na mzazi.


Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges akisisitiza jambo wakati akiteta na Wakunga nchini ambapo pia aliwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwataka kuendeleza moyo huo bila kuchoka.

Alisema hali hiyo inatokana na ukweli kuwa wazazi wenye uzazi pingamizi hucheleweshewa kufanyiwa maamuzi na hivyo kuhatarisha maisha ya mtoto na mzazi.

Wakati huo huo Rais wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga alisema ipo haja ya wakunga kujitathmini na kushirikiana ili kuhakikisha kwamba huduma wanayoitoa ni ya kiwango cha juu, inayokubalika na kuvutia.

Alisema wanawake wanapoamua kuzalia kwa wakunga wa kienyeji kuna haja ya kujiuliza kwanini wanafanya maamuzi hayo wakati vituo vipo na wakunga wapo.

Alitaka wakunga kufanyakazi zao kwa bidii na maarifa na kuhakikisha kwamba huduma zao zinakubalika ili wazazi watumnie huduma zao na hivyo kuwezesha kuwa na taifa bora.

Aidha alitaka watumie takwimu vyema katika kuboresha huduma za ukunga katika maeneo yao na hasa kuhakikisha kwamba zinafikika na zinafanyiwa kazi.


Daktari bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi, Kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Rosina Lipyoga akizungumza katika siku hiyo ya mdahalo wa wakunga ambapo alisema ni aibu kwa watoto na wazazi kufa kutokana na huduma hafifu.


Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Felista Bwana akitoa mada kwenye mdahalo huo.


Pichani juu na chini ni baadhi ya Wakunga nchini waliohudhuria mdahalo huo wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mdahalo huo.



Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy akielezea umuhimu wa Wakunga nchini kujiunga na chama hicho pamoja na faida watakazozipata pindi wawapo wanachama wa TAMA wakati wa mdahalo wa siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga duniani mjini Musoma.


Kutoka kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Christine Kwayu, Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges pamoja na Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Felista Bwana wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo.


Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Lena Mfalila (kulia) akijumuika na Wakunga kuimba wimbo wa mshikamano na hamasa mara baada ya kusikiliza risala fupi ya Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges (hayupo pichani).


Baadhi ya Wakunda kutoka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki kwenye mdahalo huo wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano.



Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA), Felista Bwana (kushoto) akishiriki kuimba wimbo huo wa mshikamano.



Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...