Skip to main content

ZIARA YA KATIBU UVCCM IRINGA







katibu mkuu wa uvccm taifa sixtus mapunda akiwapa maneno ya kishujaa wakazi wa mkoa wa iringa






juliana shonza akiwahutubia wananchi wa mkoa wa iringa








viongozi chama cha mapinduzi wakiwa katika meza wakifuatia mkutano unavyoendele



na fredy mgunda,iringa.


katibu mkuu wa uvccm taifa afanya ziara ya jimbo la kilolo kwa lengo la kukijenga chama na kuangalia maendeleo ya chama hicho hasa ngazi vijana lakini akiwa katika ziara hiyo aliongozana na mwenyeji wake katibu wa uvccm mkoa wa iringa.


akihutubia wakati wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha kitumbuka kata ya ilole katibu wa uvccm mkoa wa iringa elisha mwampashi aliwataka wanachama wa chama hicho kuondoa unyonge dhidi ya wapinzani wake kwa kuwaambia ukweli wananchi juu ya maendeleo yanayofanywa na chama hicho.


aidha mwampashe amesema kuwa ifike wakati viongizi wa chama hicho kuacha kujidanganya kwa kuwapa taarifa viongozi za matumaini juu ya maendeleo ya chama hicho.
“tunatakiwa tubadilika sasa kwa kuwapa taarifa za ukweli viongozi wetu ili wanapoondoka wajue nini cha kufanya ili kuondoa dosari ambazo zinzkuwa zikijitokeza,tuenaelekea kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapo “alisema mwampashe


kwa upande wake katibu wa uvccm taifa sixtus mapunda amewapongeza wananchi na wanachama wa tarafa ya ilole kwa ujumla kwa ushindi walioupata wakati wa serikali za mitaa ambao unaashilia chama hicho kuendelea kupendwa kata tarafa hiyo.


lakini mapunda aliwatoa hofu wananchi wa kijiji cha kitumbuka kwa kusema amesikia na kujionea baadhi ya matatizo yanayoikabili kata ya ilole na kuwaahidi kuyafikisha kwa mbunge wao na kutafuta njia ya kuyatatua kwa kuwa profesa petter msola ni msikivu.


“tatizo la kufikisha nguzo za umeme katika eneo hili ni tatizo dogo ambalo linatatulika kwa haraka na kuwaahidi wananchi kulifanyia kazi mapema ,suala la barabara alisema kuwa amejionea yeye mwenyewe kuwa si nzuri na inahatarisha maisha kwa kuwa pindi mvua itakaponyesha barabara hiyo itakuwa kama mto”.alisema mapunda.







ALIYEKUWA kada maarufu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) Taifa Juliana Shonza ambae alijiuzulu na chama hicho na kijiunga na CCM amewataka wakazi wa jimbo la Iringa mjini kuungana kulipokea jimbo kutoka kwa mbunge Mch Peter Msigwa.


Shonza ametoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mjini wakati wa mkutano wa uzinduzi wa matawi unaofanywa na katibu mkuu wa Uvccm Taifa sixtus Mapunda.


Alisema jimbo la Iringa mjini ni jimbo ambalo wananchi walichagua mbunge kwa hasira na kuwa badala ya kutegemea maendeleo wamejikuta wakifanya maandamano yasiyo na kikomo kila uchwao.


Shonza alisema kuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini amekuwa ni mtu wa kujipigania mwenyewe kimaisha badala ya kujishughulisha kuwaletea wananchi maendeleo.


Hivyo alisema ni vema wananchi wa Iringa mjini kujipanga kwa hafla ya kulipokea jimbo hilo kutoka kwa mpangaji mbunge Msigwa aliyepanga bila kujua kama kapangishwa hivyo kushindwa kulipa kodi.


Akielezea juu ya hofu ya muungano wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi (ukawa) alisema kuwa Chadema ni chama ambachokinataka kupanda kupitia ukawa.


Kwani alisema Chadema ndio chama kilichokituhumu CUF kuwa ni CCM B na kuwa ni chama cha kishoga imekuwa leo kuungana 


Hivyo kuwataka watanzania kupima na kutoa maamuzi magumu pindi uchaguzi utakapo fika.


Nae mjumbe wa kamati ya utekelezaji Uvccm Taifa Secky Kasuga alisema wananchi wa jimbo la Iringa walianzimisha jimbo hilo na sasa mwenye Nyumba anahitaji Nyumba Yake hivyo lazima mpangaji kuondoka.


"Tunalazimika kuchukua Nyumba yetu baada ya mpangaji kushindwa kufagia nyumba"


Katibu mkuu wa UVccm Taifa Sixtus Mapunda alisema kilio cha maendeleo kwa jimbo la Iringa kimetokana na mchanganyo uliofanywa na wananchi kwa kumchagua mbunge mrudisha nyuma maendeleo.


Alisema mbunge amekuwa kikwazo kikubwa kwani bungeni wakati wa vikao vya bajeti yeye anatoka nje ya bunge na wakati wa vikao vya kupanga shughuli za maendeleo halmashauri yeye anashiriki kuita maandamano.


" Tunawaombeni wana Iringa mtusaidie kurejesha jimbo kwa kumtoa mbunge mpinga maendeleo katika jimbo la Iringa mjini ambalo maendeleo yanaletwa kwa nguvu na ccm"


Bw Mapunda asema anawashangaa wapinzani kwa kuikataa katibu inayopendekezwa ambayo unazungumzia pia Haki ya kuishi hivyo kupinga Kwao wanapinga hadi haki ya wao kuishi.


Alisema kuwa hoja Yao ni kutaka serikali tatu na si vinginevyo na kuwa wananchi lazima wapigie kura ya ndio katiba hiyo na pindi muda wa serikali tatu utakapofika basi itafanyika hivyo na si sasa.


Kuwa kuutaka utanganyika ni kuutaka ukoloni hivyo lazima kujitambua kuwa wakati wa kuongozwa na wakaloni umepita.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...