Skip to main content

KATIBU WA KATA MSEKE CHADEMA AJITOSA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA MSEKE

Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Mwenyekiti wa Tawi, Haji Omary Kaguke muda mfupi ya kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya tarafa ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.

Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Mwenyekiti Wanawake Tawi la Ugwachanya, Elizebeth Marry baada ya katibu huyo kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya tarafa ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.


Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipeana mikono na Mwenyekiti wa Kata ya Mseke, Imani Lucas Ngimbe muda mfupi baada ya kumkabidhi  fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani katibu huyo leo katika ofisi ya Kata ya Mseke katika Kijiji cha Ugwachanya tarafa ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.

Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Mwenyekiti wa Jimbo la Kalenga Alex Nyulusi Kyambuke baada ya katibu huyo kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya Kata ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.

Katibu Kata ya Mseke wa Chadema, Zolango Menisy Mbwelwa (kushoto) akipongezwa na Katibu Kata (BAVICHA) Alkhan Kalolo baada ya Menisy kuchukuwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya udiwani ndani ya chama leo katika ofisi ya Mseke Kijiji cha Ugwachanya Kata ya Mlolo, Jimbo la Kalenga wilayani Iringa.



Wakiwa ofisini


MWENYEKITI wa Jimbo la Kalenga wilayani Iringa, Mkoa wa Iringa, Alex Nyulusi Kyambuko (Chadema) amewaomba wanachama na wananchi kwa ujumla kuchagua viongozi watakaochochea kuleta maendeleo katika maeneo yao kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Alisema kuwa ili chama hicho kiweze kushinda katika Uchaguzi Mkuu huo ni lazima wanachama wachague viongozi watakaochohea upatikanaji wa maendeleo.


Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi jana wakati wa  hafla ya kumkabidhi fomu ya kuomba nafasi ya kugombea udiwani ndani ya chama kwa Katibu Kata ya Mseke, Zolango Menisy Mbwelwa iliyofanyika katika  Kijiji cha Ugwachanya, tarafa ya Mlolo.

Alisema kuwa watanzania wanaotaka mabadiliko na ni wakati sasa wakujiandaa kupokea mabadiliko hayo.

Aliongeza kuwa nchi hii ina rasilimali nyingi sana lakini zinawanufaisha watu wachache kwa sababu viongozi waliopewa mamlaka ya kuzisimamia rasilimali wameshindwa kusimamia vizuri na matokeo yake umaskini unazidi kuongezeka.
“Tumeona pengo la walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka kunakopelekea wananchi wengi kukosa imani na viongozi waliopo madarakani,” alisema mwenyekiti huyo wa jimbo.

Aliongeza kuwa chama chao kina utaratibu mzuri wa kuteua viongozi wake ndio maana wanauhakika wakushinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu na kushika dola kupitia muungano wa Ukawa.

Aidha, alisema serikali watakayoiunda itahakikisha kila mwananchi anajenga nyumba bora kutoka na vifaa vya ujenzi kushuka na ndio mwisho wa nyumba za nyasi.
Alisema kuwa hawatarajii kuona wananchi wanaishi katika nyumba za nyasi baada ya vifaa vya ujenzi kama vile semeti na mabati kushika bei.
“Ili tuweze kupunguza gharama za afya kwa wananchi ni lazima wananchi wawe na makazi bora ya kuishi,” alielezea.
Kwa upande wake, mtia nia katika nafasi ya udiwani, Zolango Menisy Mbwelwa ambaye pia ni Katibu Kata ya Mseke, alisema kuwa endapo atabahatika kuteuliwa na chama kupeperusha bendera katika nafasi ya udiwani na baadaye kuchukuwa fomu Tume ya Uchaguzi (NEC), atahakikisha shule ya kata inajengwa pamoja na zahanati.
Alisema kuwa kwa muda mrefu sasa kata hiyo haina shule ya sekondari ya kata na wanafunzi wanatumia shule ya sekondari ya Tosamaganga kama shule ya kata, ambayo hata hivyo iko umbali mrefu.

Kuhusu suala la zahanati, alisema  kuwa kata hiyo haina kituo cha afya wala zahanati isipokuwa wanatumia hospitali ya misheni Ipamba ambapo alielezea kuwa huduma za afya ni kubwa kwa wananchi wa kipato cha chini.
Mwisho




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...