Skip to main content

MAONESHO YA UTALII YA SANGANAI/HLANGANANI–ZIMBABWE YAFUMBUA MACHO WATANZANIA




Pichani juu na chini ni Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)






Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.


Wageni mbalimbali waliovutiwa na vivutio vya utalii nchini Tanzania wakiendelea kumiminika katika banda la Tanzania na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) ambapo hivi sasa Shirika la ndege la Fastjet limeanza safari zake jijini Harare kupitia Lusaka hadi Dar es Salaam kwa gharama nafuu kabisa itakayowezesha wananchi wa Zimbabwe kufanya safari za Tanzania kwa gharama nafuu kabisa.


Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii zinazofanywa na kampuni yake kwa wageni waliofika katika banda la Tanzania wakati wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare.


Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (wa pili kulia) akitoa maelezo yaliyomo kwenye vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini Tanzania kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho nane ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.


Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel ya nchini Tanzania, Joseph Waryoba (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Zambia, Felix Chaila aliyembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers ambayo yamemalizika juzi.


Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tanzania Travel Company ambayo pia imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.


Timu kutoka Tanzania ambayo imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare ikiongozwa na Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba, Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (kulia).

Na Modewjiblog team, Harare

TIMU ya watanzania walioenda kuhudhuria maonesho ya utalii nchini Zimbabwe wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza uendeshaji wa sekta ya utalii.

Walisema katika ziara yao hiyo wamegundua kwamba Wazimbabwe kuanzia wanapompokea mgeni hadi anapofika hotelini wanaonesha kujali hali ambayo mgeni hawezi kusahau hata kidogo.

Aidha amesema kwamba hata mipangilio ya kwenda kwenye vivutio inafanyika katika hali ambayo huwezi kusahau hata kidogo.

Kutokana na mazingira hayo, wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza namna ya kupokea na kuishi na wageni na kuwatengenezea taswira ambayo hawatakaa wakisahau.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog yaliyofanyika mjini Harare siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers jijini Harare.

Solomon amesema ingawa hali ya Tanzania si mbaya, watendaji katika viwanja vya ndege na mahotelini wanaweza kuangalia namna Wazimbabwe wanavyojali kazi zao na tabasamu zao nyakati zote kwa wageni .

“Si kwamba kwetu kuna shida lakini unaona watu wanavyojituma hapa” alisema Esther Solomon na kuongeza kuwa aliona jinsi walivyojipanga vizuri na wafanyakazi walikuwa na uelewa wa hali ya juu.

Esther aliongoza kundi la watu watano wa Kitanzania walioalikwa na mamlaka ya utalii Zimbabwe (ZTA) kuhudhuria maonesho hayo.Tanzania iliweka banda lake pia katika maonesho hayo ya siku tatu yaliyomalizika juzi.

Makampuni ya mawakala wa utalii aliyoambatana nayo katika safari hiyo ni pamoja na Tanzania Travel Company, Cordial Tours and Travel, Mberesero Tented Camp na Best Northern Tours and safaris .

Alisema safari yao Zimbabwe pamoja na ushiriki wao katika maonesho pia walifika katika maeneo mbalimbali ya kitalii nchini yakiwemo maporomoko ya Victoria.

Aidha walipewa nafasi ya kukagua sehemu za malazi kwa ajili ya wageni.

Alisema katika maonesho hayo wamefanikiwa kupata wageni wengi wanaoulizia namna ya kufika Tanzania na pia ushirikiano wa makampuni katika sekta ya utalii.

“ Watu wengi wamekuja kututembelea. Na wengi ni watu weusi. Mwamko wao wa kutembelea vivutio ni mkubwa.” Alisema Esther na kuongeza kuwa wamebaini kwamba ipo haja ya watanzania kuhimizwa kutembelea vivutio kwani hata nchini Zimbabwe wanaotembelea vivutio ni wananchi wenyewe.

Alisema wengi waliofika katika banda la Tanzania waliulizia namna ya kufika visiwa vya Zanzibar na pia mbuga za Tanzania.

Aidha mawakala wengi waliulizia namna ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utalii katika bara la Afrika.

Asilimia 80 ya watalii nchini Zimbabwe wanatoka bara la Afrika na waliobaki ndio wanatoka nje ya bara hili.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...