Skip to main content

Mwanasheria wa Chadema Lucas Sinkala Mwenda ajitosa ubunge Jimbo la Kalenga



Mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya ya Iringa, Anjelika Kihakwi akibadilishana mawazo na kada mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Kijiji cha Ihomasa Kata ya Wasa, Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa. Chadema walifanya mkutano wa hadhara jana katika kijiji hicho kwa lengo la kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha watia nia waliotangaza kugombea kubunge Jimbo la Kalenga.


Kada wa CHADEMA na Mwanasheria wa chama hicho, Lucas Sinkala Mwenda (kulia) ambaye ametangaza nia kugombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho amechukua fomu kwa Katibu wa CHADEMA Jimbo la Kalenga, Issa Nyamahanga jana katika Kijiji cha Ihomasa kata ya wasa Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa.  

Mkazi wa Kijiji cha Ihomasa Kata ya Wasa, Mzee Gaudencia Chogavanu Kikoti akiuliza swali kuhusu michango ya ujenzi wa maabara inayoendela kuwa ni mkubwa kulingana na hali zao za maisha kuwa duni, ambapo kila nyumba ina lazimika kutoa shilingi 30,000/- waktika wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana. Mkutano huo wa chama ulilengo kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha watia nia kwa wananchi Jimbo la Kalenga wilayani Iringa, mkoani Iringa.


Watia nia kugombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA, Mwanasheria wa chama hicho, Lucas Sinkala Mwenda (kushoto), Grace Tendega na Mussa Mdede wakiwasalimia wananchi wa Ihomasa, Kata ya Wasa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana. Mkutano huo cha walikuwa kwa lengo la kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha watia nia kwa wananchi.


Hatimaye kada wa Chadema na mwanasheria msomi Lucas Sinkala Mwenda amechukuwa fomu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kugombea ubunge kwa mara ya pili kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.


Mwenda aliyekuwa mgombea kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga ambaye  aliyewashinda wagombea  wengine 12 katika kura za maoni ndani ya chama alipokwa ushindi  na chama hicho na  kikamteua mshindi wa pili Grace Tendega kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo huo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimtaja mgombea huyo kuwa ni Grace Tendega. Mbowe alisema kuwa, awali vyombo vya habari vilikuwa vimemtangaza Lucas Mwenda kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo, jina ambalo halikuwa limepewa baraka na Kamati Kuu yenye uamuzi wa mwisho.

Akifafanua zaidi, Mbowe alisema kuwa ingawa Lucas Mwenda alipata kura 132, Kamati Kuu imempitisha Grace Tendega aliyepata kura 122.

Akizungumzia sifa za Mwenda, Mbowe alisema: “Bwana Sinkala (Mwenda) bado kijana mdogo, mwanasheria wetu na tunahitaji kumkuza zaidi, basi vyombo vyote vimeshauri nafasi hii apewe mama Tendega kwa sababu ana sifa za kutosha,” alisema Mbowe.

Alifafanua kuwa uchaguzi uliofanyika Iringa ulikuwa ni sehemu tu ya vigezo vinavyotumiwa na chama kumpata mgombea mwenye sifa na ushawishi kwa wanachama wake.

Mwenda amekabidhiwa fomu hiyo jana na Katibu wa jimbo la Kalenga, Issa Nyamahanga wakati mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Ihomasa Kata ya Wasa, wilayani Iringa, Mkoa wa Iringa.

Mkutano huo ulilenga kukagua uhai wa chama pamoja na kuwatambulisha baadhi ya watia nia kupitia wa chama hicho akiwemo Grace Tendega, Mussa Mdede na Lucas Sinkala Mwenda ambao idadi yao inafika jumla watangania wanne waliochukua fomu mpaka sasa.

CHADEMA katika uchaguzi wa kujaza nafasi ya Ubunge jimbo la Kalenga-Iringa lililoachwa wazi na marehemu Dk.William Mgimwa, waliojitokeza kugombea na kura zao ni hawa wafuatao, Zuberi Mwachula – kura (0), Mch.Samwel Nyakunga - kura (2), Aidan Pungili - kura (2),Daniel Luvanga - kura (1), Rehema Makoga - kura (4), Henri Kavina - kura (9), Vitus Lawa - kura (12), Akbal Sanga -kura (21), Anicet Sambala - kura (22), Dk.Evaristo Mtitu kura (32), Musa Mdede - kura (48), Grace Tendega - kura (122),Lucas Sinkala Mwenda - kura (132).

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...