Skip to main content

AFRIKA KUSINI YAKABILIANA NA TABIANCHI KWENYE MIJI YAKE MIKUBWA



Mkufunzi na mtafiti, Daktari John Odindi, kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban nchini Afrika Kusini (kulia) katika mahojiano maalum na mwandishi wa Habari mwandamizi wa modewjiblog.com, Andrew Chale kwenye mkutano wa wanasayansi juu ya mabadiliko ya tabianchi, unaoendelea kwenye ukumbi wa Makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa (Picha na Mpiga picha maalum)

[Paris, Ufaransa] Watafiti kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban nchini Afrika Kusini wamewasilisha mada juu ya mabadiliko ya tabianchi kuhusiana na ongezeko la joto kwenye miji (urban temperature increase) ya Durban, East London na Port Elizabeth kwenye nchi hiyo.

Mada iliyowasilishwa na Daktari John Odindi katika mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’ unaofanyika kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa. Mkutano huo wa siku nne (Julai 7-10) unawajumuisha wanasayansi zaidi ya 2500 kutoka pembe zote duniani.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Dk. Odindi ambaye ni mkufunzi na mtafiti anasema hali ya ongezeko la joto ni kubwa na kupitia utafiti huo wanashauri jamii kuchukua hatua dhidi ya kukabiliana nayo.

“Utafiti wetu tuliowasilisha ni tumeangalia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi dhidi ya joto katika miji hii kwani linakuwa kubwa kutokana na ongezeko la makazi mengi ya watu, viwanda na shughuli za kila siku za wananchi” alibainisha Dk. John Odindi.

Dk. John Odindi anashauri uhifadhi na utunzaji wa mazingira ya asili ikiwemo mimea, chemichemi za maji ya asili na mito kulindwa kwani vitu hivyo ndivyo vinavyosaidia kupunguza hali ya joto mijini.

Hivyo ansema kupitia mkutano huu wa Wanasayansi, kuelekea mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21) utakaofanyika Paris , Desemba mwaka huu, anatumai kwamba mataifa yatajumuika kutafuta muafaka za kupunguza kiwango cha joto duniani.

Pia anabainisha kuwa, nchi ya Afrika Kusini imejidhatiti katika kukabiliana na hali hiyo ya tabianchi katika ongezeko la joto mijini kwani mkutano wa COP17, ulifanyika katika jiji la Durban, Afrika Kusini.

Mada hiyo inaenda sanjari na matakwa ya mataifa mbalimbali juu ya kukabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to reduce temperature level by 2 degrees).


Baadhi ya wanasayansi hao wakiwa katika mkutano huo unaendelea katika ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa.. (Picha kwa hisani ya Christophe Maitre, INRA).


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...