Skip to main content

MODEWJIBLOG YANG’ARA MAONYESHO YA SABASABA HUKU IKITIMIZA MIAKA 7






Pichani juu na chini ni Meneja Mwendeshaji wa tovuti ya Modewjiblog, Zainul Mzige akiwapa ufafanuzi wadau waliotembelea banda la tovuti hiyo lililopo MeTL Pavillion katika maonyesho ya kimataifa ya kibiashara ya Sabasaba yanayoendelea katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Bw. Zainul pia ametumia fursa hiyo kutaja umri wa tovuti hiyo ambapo amesema sasa inatimiza miaka saba(7) tangu ilipoanzishwa na kuwa inatarajia kuadhimisha “birthday”itakapofika mwezi wa tisa mwaka huu na amewataarifu wadau kukaa mkao kujiachia. 

Na Modewjiblog team

Tovuti mahiri ya habari ya modewjiblog leo imevuta umati wa watu wanaotembelea maonyesho ya 39 ya kimataifa ya kibiashara Sabasaba katika banda lake lililopo MeTL Pavillion.

Wengi kati ya watu hao walikusanyika kutaka kujua ni jinsi gani tovuti inavyofanyakazi kwa haraka na usahihi sambamba na picha za matukio yanayokuwa yamejiri kwenye habari husika.

Akitoa maelezo kwa kina Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Bw. Zainul Mzige amesema ni kutokana na uelewa wa watendaji wa tovuti hiyo na kujituma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na wananchi wote kwa ujumla.

Akitoa maoni yake wakati alipotembelea banda la Modewjiblog, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema amesema anafurahishwa sana na habari zinazoandikwa na tovuti hiyo na kuwa yeye ni mdau mkubwa kwani kila siku lazima aitembelee ili kujua dunia inaendaje.

Aidha tovuti hiyo imewataka watu wafike katika maonyesho hayo kutembelea katika banda lake ili kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali wanayotaka kujua kuhusu Modewjiblog na pia kutoa maoni yao.














Mrembo wa Modewjiblog, Josephine Emilian, akisimamia zoezi la wadau kutia saini kwenye kitabu cha wageni.


Mrembo wa Modewjiblog, Josephine Emilian akitoa kipeperushi kwa wadau waliotembelea banda letu.


Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Modewjiblog katika maonyesho ya sabasaba.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...