Skip to main content

ZAIDI YA WATU 600 WATOA MAONI JUU YA UTENDAJI KAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI


IMG_7241
Pichani ni muonekano wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania ndani ya Karume Hall katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, ndani ya viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Pichani ni wananchi wakitembelea banda hilo na kupata taarifa mbalimbali za shughuli za Umoja huo nchini Tanzania.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_7256
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa mwananchi katika picha za viongozi mbalimbali waliowahi kuwa Makatibu wakuu wa Shirika la Umoja Mtaifa duniani ambalo hivi sasa linaongozwa na Ban Ki-Moon.
IMG_7248
Pichani juu na chini ni Ismael Mnikite (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, ndani ya viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_7259
IMG_7264
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati) akifafanua jambo kwa mdau wa Umoja wa Mataifa, Shaweji Steven (kushoto) aliyetaka kujua zaidi kuhusiana na ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika tatizo la ajira za vijana nchini. Kulia ni Emmanuel Johnson kutoka Shirika la Afya (WHO) nchini.
IMG_7253
Ismael Mnikite (kulia) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akitoa darasa la Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDG's) yanayotekelezwa na nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa ambapo Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi wananchama kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda hilo lililopo Karume Hall katika maonyesho ya Sabsaba.
IMG_7221
Emmanuel Johnson (kulia) kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) nchini akitoa maelezo ya ripoti ya UNDAP kwa mdau wa Umoja wa Mataifa, Shaweji Steven alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba lililopo Karume Hall.
IMG_7213
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) na Salome Mwambinga (wa pili kulia) kutoka (IAEA) wakihudumia wananchi waliotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimu vumbi jijini Dar.
IMG_7237
Wananchi wakisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa.
IMG_7235
Wananchi wakijichukulia vipeperushi mbalimbali vyenye taarifa za shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Na Modewjiblog team
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu, amesema tangu Umoja huo ulipotoa fursa kwa wananchi wanaotembelea maonyesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya sabasaba kutoa maoni kuhushu utendaji wake hapa nchini mpaka sasa zaidi ya watu 600 wameshiriki kutoa maoni yao.
Amesema watu waliotoa maoni hapo wametumia njia tofauti ikiwemo mtandao, ujumbe mfupi wa maandishi (sms), njia ya mdomo na kwa kuandika katika fomu maalum zinazopatikana katika banda lao
Bi. Temu amewashukuru wote walioshiriki kutoa maoni yao na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano pia katika mambo mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa nchini.
Jinsi ya kuendelea kushiriki kutoa maoni kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055 bila makato yoyote kwenye simu yako.
Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni yako moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...